Chocolate Zinavyohusishwa na ‘Uwezo wa Akili’ Kwa Wanafunzi Darasani
Wakati wazazi wengi nchini wakihaha kudhibiti ulaji holela wa vitu vitamu kwa watoto wao ili kuimarisha afya ya kinywa. utafiti mpya wa hivi karibuni umeibuia mapya baada ya kubainika kuwa ulaji mzuri wa chocolate unaweza kuongeza uwezo wa kufikiri na hivyo kutoa fursa kwa watoto kufanya vizuri darasani. Aidha, utafiti huo umebaini vilevile kuwa ulaji wa chocolate husaidia kupunguza kasi ya kawaida ya kuzeeka kwa walaji itokanayo na kuongezeka kwa umri. Ripoti ya utafiti huo ilitolewa hivi karibuni, inabebwa na utambulisho usemao ‘ulaji wa chocolate huongeza utendaji kazi wa ubongo” na kwamba ”unaweza kusaidia mtu kutozeeka haraka licha ya umri kuzid kumtupa mkono’ Utafiti huo uliochapichwa mwezi huu katika jarida la Appetite, umebaini kuwa kumbukumbu na uwezo wa kufikiria ufumbuzi wa mambo magumu kuwa katika kiwango cha juu kwa watu wanaokula chocolate kwa wingi. Matokeo hayo yameripotiwa kutoathiriwa na umri wa mlaji, uzito wa mwili wala aina nyingine za ulinganifu wa ...