Posts

Showing posts from October, 2016

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Image
Dalili za Mke anayetoka nje ya ndoa: 1) Anatembea na vidonge vya majira kwenye mkoba wake, wakati mume amefanyiwa Vasectomy (Kufunga kizazi kwa mwanaume) 2) Anakuwa na namba ya siri ya simu ambayo mume haijui 3) Anatumia muda mwingi anapokwenda sokoni au kufanya manunuzi ya wiki 4) Anajinunulia nguo za gharama zikiwemo nguo za ndani bila kumshirikisha mume 5) Anakuwa akitegemea zaidi ushauri kutoka nje kwa watu wengine zaidi ya mumewe 6) Anaacha kuvaa pete ya ndoa bila sababu 7) Anapopigiwa simu akiwa karibu na mumewe anaizima au kwenda kupokelea nje 8) Anakuwa hajali tena mambo ya familia na hujiamulia mambo yake mwenyewe 9) Ni rahisi sana kusema ‘nipe talaka yangu’ inapotokea kutofautiana hata kwa jambo dogo. 10) Dharau na kejeli kwa mume hujionyesha waziwazi Dalili za mume anayetoka nje ya ndoa: 1) Unakuta Condom kwenye mkoba wake au kwenye gari lake wakati umefunga kizazi au unatumia vidonge vya majira. 2) Anapunguza au anaacha kabisa kuwa outing na fa...

Vanessa Mdee Afichua Sababu za Ali Kiba Kuzimiwa Mic Mombasa

Image
Vanessa mdee ambaye pia ali pafomu Mombassa ametaja sababu iliyosababisha Ali Kiba kuzimiwa mic ni kuwa Chris Brown aliingia akiwa hana mood nzuri, kwa hivyo ili kumfurahisha wale waandaji ikabidi wakatishe shoo ya Ali Kiba wampe muda wa kupanda jukwaani atakapojisikia yeye                                                           

Nyumba Aliyosema Barakah The Prince Anajenga ni ya Mama yake Naj, Kwa Mujibu wa Msanii Aliyeoa Kwa Akina Naj

Image
Kwa wengi haikuwa rahisi kuamini maneno ya Barakah The Prince kuwa anamalizia kujenga mjengo wake aliouonesha kwenye Instagram. Ni kwa sababu ujenzi si suala la lelemama na linaloweza kutokea kwa usiku mmoja. Pia wengi walitia shaka uwezo wa msanii huyo katika kipindi hiki kuweza kujenga nyumba kama hiyo. Na sasa huenda mashaka hayo yakawa yamepata uthibitisho wa uhakika. Alawi Junior (katikati) akiwa na shemeji yake, Naj (kushoto) mwenye uhusiano na Barakah Ni kutoka kwa Alawi Junior – msanii wa Bongo Flava aliyemuoa na kuzaa na dada yake Naj, Lady Naa. Alawi amepost Instagram video ya nyumba ambayo Barakah alidai ni ya kwake na kuandika: Done🏠👍Hongera sana Mama mkwe #zaharaDattan nyumba yako kali sana.” Cha kufurahisha ni kuwa Barakah na mpenzi wake Naj Dattan walihojiwa na EATV na wote kuthibitisha kuwa ni nyumba ya Barakah! “Namshukuru sana mke wangu Naj kwa sababu ana mchango mkubwa sana hadi hapa nilipofika pia kwa sasa siwezi kutaja fedha a...

Stan Bakora Ajibu Mapigo Kwa Barakah The Prince

Image
Mchekeshaji maarufu Stan Bakora amefunguka juu ya povu lililomtoka Barakah The Prince siku kadhaa baada ya kuachia parody ya wimbo ‘Nisamehe’. Kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Stan amesema kuwa kama asingefanya vile video ingekuwa ya kawaida tu na isingeleta maana. Barakah ameshindwa kuelewa. Kama nisingefanya vile ile video isingeleta maana, lazima uonyeshe uhalisia. Kwani Baraka si mweusi kweli?,” amesema Stan. Stan aliendelea kwa kumtania Barakah kwa kumwambia kuwa hapa mjini [Dar es Salaam] ndio kwanza ana Christmas mbili. Awali baada ya Stan kuachia parody hiyo, Barakah aliandika kwenye Instagram: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.”