Nilivyofanya Bonge la Sherehe Baada ya Mke Wangu Kufukuzwa Kazi
Huyu mke nilimuoa akiwa hana kitu, kwa bahati alitafutiwa kazi na ndugu yake kwenye kampuni moja ya simu akawa analipwa kama milioni 3 kwa mwezi fasheni na yeye yeye na fasheni vipodozi kila aina,handbag na nywele za laki mbili ndio mshahara wake ukawa unaishia huko mimi mshahara wangu hauzidi laki sita,nilifanyishwa vituko vyote ndani ya nyumba ,manyanyaso yote ,hapiki hafui,hafanyi chochote ndoa ikawa inaelekea kuvunjika. Nikaenda mahakamani kuprocess talaka wakasema mpaka nianzie baraza la usuluhishi la kata au kanisani,nikaamua kwenda kanisa tulilofungia ndoa tukaitwa kwa Baba Paroko for hearing sijui mediation sijui arbitration sijui mie nikatinga kwa bajaj ya kukodi nimepaukaaa yeye akaja na RAV4 . Baba Paroko alivyotusikiliza akaaniita pembeni akasema kijana hapa nadhani hata tukiomba na kukariri mistari yote ya biblia plus mapambio yote ndoa yako haitarudi kama mwanzo pambana utafute hela ,huyu ni mchaga katumwa pesa mjini Nilisali sana nikasugua g...