Kwa mujibu wa mtoa ubuyu wetu makini, Kabula alitaitiwa na polisi usiku wa Jumatano iliyopita mara baada ya kutendo kosa hilo walipokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar wakitazama mechi kati ya Yanga na TP Mazembe ya DR Congo.
“Walipishana kauli kule uwanjani, si unajua Kabula ni Yanga damu, sasa nahisi alishindwa kustahimili utani wa Stella ndipo akamporomoshea matusi ambayo yalimfanya mwenzake akimbilie polisi.
“Alikwenda kushtaki Polisi Kijitonyama (Mabatini), akapewa polisi na kwenda kumkamata Kabula ambaye wakati huo alikuwa kwenye sherehe ya mtoto wa Esha Buheti. Wakamtia ndani hadi kesho yake (Jumatano) walipomtoa kwa dhamana,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunasa ubuyu huo, Jumatano iliyopita, Risasi Jumamosi lilimtafuta Kabula ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo ambapo alikiri kutokewa na tukio hilo na kudai wameshamalizana.
“Ni kweli ilikuwa hivyo lakini tumeshamalizana kiutu uzima, yamekwisha tayari,” alisema Kiba.
Alipoulizwa Stella, aliahidi kufafanua kwa ujumbe mfupi (SMS) tukio hilo lakini hadi tunakwenda mitamboni, hakutuma.
Comments
Post a Comment