Posts

Showing posts from June, 2016

Gigy Money Atangaza Kumuacha Buzi la Kiarabu Sababu ni Bahili...

Image
VIDEO Queen asiyeishiwa vituko, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amethibitisha kuwa yupo mbioni kumpiga kibuti bwana’ke mwarabu endapo ataendelea kuwa bahili, kwani kwake yeye hakuna mapenzi isipokuwa anachojali ni hela tu. Akichonga na Risasi Mchanganyiko, Gigy Money alisema katika maisha yake hapendi mwanaume bahili wala asiye na fedha hivyo kwa kuwa mwarabu huyo ambaye awali alikuwa akimpatia hela nyingi, na sasa anaonekana kumbania kumpa mshiko, atamtosa muda si mrefu ujao. “Siku hizi hakuna mapenzi ya kugandana, mapenzi ni hela, mimi mwenyewe sina hela halafu nikampende mwanaume kapuku tutaendeshaje maisha sasa? Huwa sifanyi biashara hiyo, kikubwa kwangu nampenda mwanaume mwenye mkwanja, mwarabu anazo na mwanzoni alikuwa akinipa za kutosha, lakini sasa naona amekuwa bahili, namuacha,” alisema Gigy Money.

Mr. Blue: Mimi Ndio nilimtoa Alikiba, Bangi ilisababisha nidrop kimuziki

Image
Mr. Blue amesema kuwa yeye ndio aligundua kipaji cha Ali Kiba na kuamua kumpeleka studio. Pia ameongeza na kusema kuwa alikuwa anavuta sana bangi ndio sababu kubwa iliyomfanya ashuke kimuziki. Tazama Video Hapa Akifunguka:                                              

Suluhisho Rahisi Kwa Wanaodhani Wamepungukiwa Nguvu, Wanaosumbuka Kurudia Tendo au Kuwahi Kufika

Image
Inavyoonekana siku hizi japo kweli kuna tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haswa kwa mazingira ya mijini, Lakini hili tatizo linaonekana kukuzwa kuliko lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa baadhi ya wengi wetu. Kwa kuanzia yafuatayo yaweza kusaidia kuboresha kulifurahia tendo la ndoa zaidi na kwa muda zaidi. Kuuweka Mwili vizuri: Ni wazi kuwa tendo hili linachagiwa sana na mzunguko mzuri wa damu. Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia. Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki. Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla ya kuendelea na awamu nyingine. Japo kuna ambao ...

Ukweli Kuhusu Kupata Watoto Mapacha na Jinsi Wanapatikana

Image
Inasemekana kwamba haijalishi kama mume/mwenza wako ni pacha ama ametoka kwenye familia yenye historia ya mapacha. Mwenye uwezo wa kusababisha watoto mapacha ni mwanamke pekee. Ikiwa na maana mwanamke ambaye ni pacha ama ndugu zake wa kike kama vile dada, mama wana historia ya kuwa na mapacha ama wao ni pacha basi mwanamke huyo ana nafasi kubwa ya kupata watoto mapacha. Kwa mfano: Mwanamke ambaye mke wa mjomba wake ana mapacha haimpi yeye nafasi ya kupata mapacha kwa sababu hana uhusiano na mke wa mjomba wake kibailojia. Ila mwanamke ambaye dada yake ana mapacha inampa uwezekano wa kupata watoto mapacha kwasababu wana uhusiano wa moja kwa moja. Hembu tujifunze hatua moja baada ya nyingine. Kwanza tufahamu mimba inatungwa vipi? Na kisha tuone jinsi gani mimba ya watoto mapacha inavyotungwa. Mimba inatungwaje? Kipindi cha ovulation ndipo ambapo mwanamke anaweza kushika mimba. Ovulation ni kipindi ambacho yai kubwa ama yai lililo tayari hutoka kuelekea kw...

Mahaba ya Harmozine kwa Wolper: Siku zinavyozidi Kwenda Nazidi Kukuona Mpya

Image
Hit maker wa ‘Bado’ Harmonize anaendelea kuudhirishia umma jinsi anavyompenda baby mama wake Jacqueline Wolper. Muimbaji huyo amewaziba mdomo mashabiki ambao wanabeza uwamuzi wake wa kutoka kimapenzi na mwanamke aliyemzidi umri. Harmonize alipost picha ya Wolper instagram na kuandika: Get well soon mami….🙏 siku zinavyozidi kwenda nazidi kukuona mpya…..!!! hivi kina miaka ngapi hiki kitoto …..??? 13 au 14 mana nami kwa kusahau. Kauli hiyo imeonyesha kuwatoa povu baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii. Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao. Alwatan_de_don Sikuzote MTU akikosea njia ndo anajifanya haoni eti umri wake miaka mngapi,,,,😁😁 vijimambo hv Neema3071 Heshima pesa shikamoo makelele age namba tu lkn ukimchek kama anamiaka20 hiv matuzo tu poleen wenye majungu hendrickanthony2016 Kwan miaka its just a number hats Bibi kizee anaweza akampenda mtoto wa miaka mi5, mapenz hayajal umri its a Mata of loving each other,,, nakupenda bro ...

Fella: Mwanamuziki Ruby Ana ‘stress’ Ndio Maana Hajaonekana Kwenye Video Yamoto Band

Image
Ruby alikuwa ana ‘stress’ ndio maana alishindwa kutokea kwenye video ya wimbo SU wa Yamoto Band alioshirikishwa. Meneja wa kundi hilo, Said Fella amekiambia kipindi cha E News cha EATV kuwa hiyo ndio sababu aliyokuwa akipewa na Ruby. Amedai kuwa baada ya kuona kuwa Ruby amekuwa akitoa sababu hiyo kwa muda na hawakutaka asishiriki akiwa hana mood, walilazimika kuifanya bila yeye. Kwenye video hiyo anaonekana msichana mwingine akiimba sehemu ya Ruby. Haijafahamika mara moja ni mambo gani yanamsibu muimbaji huyo kiasi cha kumpa msongo wa mawazo lakini kwa wanaofahamu, stress ni kitu kinachoweza kukuondelea mood ya kufanya vitu vingi.

Wabunge Wataka Clouds Tv Iadhibiuwe Kwa Kufanya Mahojiano na Kijana Ambaye ni SHOGA

Image
WABUNGE wameiomba serikali kukichukulia hatua kituo cha televisheni, Clouds Tv nchini kwa kukiuka maadili na taaluma ya habari kwa kurusha kipindi ambacho maudhui yake yalikuwa ni kutangaza mapenzi ya jinsia moja. Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) aliomba Mwongozo kuhusu kurushwa kwa kipindi ambacho kilikuwa kikimhoji kijana mmoja ambaye anajihusisha na vitendo vya ushoga. “Napenda kuweka maslahi yangu kuwa mimi mwenyewe ni mwanahabari na taaluma hii naifahamu na ndio maana nikaona ni vyema nisimame angalau kupata muongozo wako,” alisema Mollel na kuongeza kuwa sheria ya nchi hairuhusu ushoga kwa maana hiyo kama mwandishi wa habari alipaswa kuzungumzia ushoga, basi angeelimisha jamii kwa kuonesha kuwa kijana huyo anajutia kufanya vitendo hivyo. Alisema mwandishi huyo angefanya hivyo ili kutoa taarifa kwa wengine kwamba vitendo hivyo sio vizuri katika jamii badala yake kipindi kilihamasisha vitendo vya ushoga na alionesha ni mtu anayefurah...

Fisi Amng'ata Mtoto Afrika Kusini

Image
Maafisa wa mbuga ya wanyamapori nchini Afrika Kusini wamewashauri waweni kuwa makini, baada ya fisi kumshambulia mtoto wa umri wa miaka 15 alipokuwa amelala ndani ya hema katika mbuga ya Kruger. Msemaji wa mbuga za wanyamapori William Mabasa, aliwashauri wageni kuchukue tahadhari kila wakati, kwa kuwa kuna wanyamapori wanaowazunguka, na kuwataka wahakikishe kuwa hema zao zimefungwa vizuri. Mtoto huo alifanyiwa upasuaji ili kupata matibu kwenye mdomo, kutokana na majeraha aliyoyapata kufuatia shambulizi hilo.

Msinifananishe na Mal*ya Ambao Hawajawahi Kwenda Labour Kujifungua – Zari

Image
Nani amemchokoza Zari? Kwasababu kwa kile alichokipost kwenye mtandao wa Snapchat inaonekana ameguswa pabaya na amemind! Najua unajiuliza kwanini hajapost Instagram – ni kwasababu kwa alichokiandika, povu lake lingekuwa la haja! Snapchat ya kishua, mastaa wako huru kusema chochote na hakuna povu kama mitandao mingine. Amesema nini? “Na wengine acheni kunifananisha na mal*ya ambao hawajawahi kwenda labour,” aliandika. “Mtoto mmoja tu kwenye labour na watakaonekana kama tikiti maji lililopasuliwa. Acheni!” “Nikiwa na miaka 35 na watoto wanne, badi mimi ni mrembo mno kunifananisha, naomba.” Tazama kwa picha alichokiandika:

Lulu Michael Kushtakiwa Kwa Makosa ya Mtandao....

Image
Dar es Salaam: Mwigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ yupo mbioni kupambana na mkono wa sheria kufuatia kumvurumishia matusi mwandishi wa habari wa Global Publishers baada ya kumuuliza swali lililotaka ufafanuzi wake ikiwa ni siku chache tangu alipofanya hivyo kwa mwandishi mwingine wa kampuni hiyo. Ishu hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita ambapo paparazi alimtwangia simu ya mkononi Lulu na kumuuliza kuhusu kuwepo kwa madai kwamba, yeye ni mjamzito na amekuwa akishinda ndani kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa chanzo chetu, msanii huyo kwa vile sasa ni mama kijacho, amekuwa nadra kuonekana sehemu za hadhara kwa kuwa hataki watu wajue kwa kuwahofia wabaya wake. “Ndo’ maana sasa kumuona Lulu waziwazi ni ngumu sana, naona yeye na aliyempa mimba (hakumtaja) wamepanga hivyo. Si unajua wambeya wengi, nadhani anahofia macho ya watu wenye vijiba vya roho na wale washirikina, wakimuona isije mimba ikachoropoka kabla ya wakati,” kilisema chanzo hicho. Sasa kufu...

Barakah Da Prince Afungukia Ujauzito wa Najma Kumkwamisha

Image
MSANII mwenye ‘title’ kubwa kwa sasa ndani ya ardhi ya JPM, Barakah Andrew ‘Barakah Da Prince’ amekanusha juu ya tetesi zinazoendelea kuwa mpenzi wake Najma ni mjamzito na kwamba ujauzito huo ndiyo unaomfanya yeye kushindwa kuachia kazi nyingine. Akizidi kufungukia tetesi hizo Barakah aliongeza kusema kuwa alipanga kuachia kazi mwanzoni mwa Julai lakini ameshindwa baada ya kupata menejimenti mpya na kwamba kwa sasa kuna baadhi ya mambo wanayaweka sawa hivyo anatarajia kuachia kazi mpya Agosti.  “Kuhusu Najma kuwa mjamzito kwa kweli hizo taarifa sifahamu na kama upo utaonekana tu maana hicho kitu huwa hakijifichi, hata hivyo wapenzi wa kazi zangu naomba waamini kuwa nipo katika mipango mizuri ya kazi kwa sasa na Agosti siyo mbali, nitatoa kazi nzuri itakayokidhi vigezo vya kimataifa,” alisema Barakah. Aliongeza kuwa, kwa sasa hayuko tayari kuifungukia menejimenti hiyo mpya inayosimamia wasanii wawili wakubwa kutoka nchini na wengine wa kimataifa. ...

Utajiri wa Diamond Umefikia Shilingi Bilioni 8.6

Image
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani. Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6. Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber. Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo y...

TID amlalamikia Billnass, ‘sijapenda alikuwa akinibembeleza nimsaidie ajulikane’

Image
Msanii wa muziki na Mkurugenzi wa kundi la Radar Entertainment, TID ameingia kwenye mgogoro na rapper Billnas aliyekuwa member wa kundi hilo kabla ya kutimkia katika label mpya ya ‘LFLG’. Mapema mwaka huu Billnas aliiambia Bongo5 kuwa aliondoka Rada bila matatizo na mtu yeyote. Akiongea na Clouds Fm, TID amedai Billnass amesahau alikotoka na hatoi heshima kwa watu walio msaidia kumfikisha hapo alipo sasa. “Mi sijapenda alikuwa akinibembeleza nimsaidie ajulikane, alikuwa ana nidhamu lakini sasa hivi hanipigii simu, tukimwambia afanye hivi hataki,” alilalamika TID. “Why do we help people who do not help us, why he think he is on top all over the sudden no!! People don’t live like that… People need to respect the people who help u… And of the day,” Aliongeza, “Mimi i gave out to my heart, my voice, my energy, my talent to make him shine but I don’t see any effort, hajanipa hata laki moja kuniambia nashukuru, anafanya tour hata kuniambia Mzee Mnyama chukua hii laki tano...

Mwanaume Aoa Wanawake Wanne Kwa Siku Moja...

Image
Kuwaiti guy, 28yrs old, married 4 wives in one wedding after his ex dared him if he could find one woman to marry him! In a measure to show his ex-girlfriend that he could do “better”, a 28-year-old man from Kuwaiti married four wives in one wedding. Tazama Video:

Nimegundua Wanawake wengi (85%) Wanateseka Sana Ndani ya Ndoa....Embu Zindukeni.....

Image
Hili jambo limeniuma sana tena sana, wanawake wengi wanaonewa na waume zao bila kusema popote wakijua ndio kuvumilia kumbe hawajui wanajiua pasipo kujua inaniuma sana. Nimeongea nawanawake zaidi ya 20 walio wengi hawana raha ya ndoa au tuseme tuu ya maisha wanasema wanavumilia huku miaka inaenda wakiwa ndani ya mateso makali, Kama kulea familia wenyewe bila kusaidiwa na baba hata senti, kufungiwa nje bila huruma yani kufukuzwa, kutukanwa na kudharauliwa, kupigwapigwa hivyo hata kuachiwa ulemavu, kubebeshwa mzigo wa kulea watoto wenyewe au kutelekezewa watoto mwanaume akapotea kabisa nyumbani baada ya miaka kumi hadi ishirini ndio anarudi na watoto wanamfurahia bila mama kufanya lolote, wanaume 98% kutokuwa waaminifu ndani ya ndoa zao, kuambukizwa magonjwa ya zinaa na ukimwi, na kugeuzwa kuwa punda wake bila huruma, kwakweli hili jambo limeniuma sana wanaume walio wengi ni mashetani wanaigiza kuwa binadamu hivyo kupelekea wana wake kufa haraka. Wanawake embu zinduke...

Joyce Kiria ‘Superwoman’ wa Wanawake Live Apata Ajali

Image
Mtangazaji wa TV, Joyce Kiria pamoja na crew ya kipindi chake, Wanawake Live, wamepata ajali wakati wakielekea mjini Sumbawanga, Rukwa. “Juzi jtano tulianza safari ya kuja Sumbawanga toka kwa lengo la kumtembelea Wankota Binti Shujaa asiekata Tamaa kirahisi wala asieogopa changamoto, na pia ilikuwa tukitoka kwa Wankota, ni safari ya kwenda Mbeya kufanya kampeni ya Mwanamke Piga Kazi kesho jmosi kisha ndo tugeuze kurudi dar….. Leo mapema ndo tumeingia Sumbawanga, lakini kwa bahati mbaya tumepata Ajali tukiwa kijiji cha pili toka kwa kina Wankota….yaani tulikuwa tumebakiza km 20 kati ya km1500. Tunamshukuru Mungu sana tumepona maana ndo kikubwa,”  Joyce ameandika  kwenye ukurasa wake mtandaoni.                                           

Umaarufu wa Supu ya Pweza Kwa Wapwani..Je ni Kweli Inaongeza Nguvu za Kiume?

Image
Ukitembea katika mitaa ya Mombasa na Pwani kwa jumla, utaskia wakaazi wakisema wametoka kunywa supu ya pweza. Licha ya kwamba wengi wanamfahamu mnyama huyo wa majini kama kitoweo, umuhimu wa mnyama huyo kwa wapwani ni mkubwa mno baada ya wao kugundua kuwa ana faida zaidi katika maisha ya kila siku. Wataalam wa sayansi wamedhibitisha kwamba nyama ya pweza pamoja na supu yake inaongeza madimi muhimu kwa binadamu, na la kuvutia zaidi ni kwamba husaidia kuimarisha nguvu za kiume. Wanaume haswa hupenda kuitumia huku wakiamini kwamba inawasaidia kuwapa nguvu wakati wa kufanya mapenzi na wake wao. Nilikutana na baadhi ya wavuvi mjini Mombasa na kutaka kujua ni kitu gani kinafanya supu ya pweza kuwa maarufu sana kwa wakaazi wa eneo hilo. “Hapa Mombasa ukisema umetoka kunywa supu ya pweza utashangaa watu wakikuangalia mara mbili. Uwa tunaamini kwamba inaongeza nguvu za kiume na hii ndio sababu huwa tunapenda kuitumia,” alisema Omari, mmoja wa wavuvi hao. Wakaazi hao walisema ...

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!

Image
Kabla ya kuanza makala hii, ni muhimu kujua kwamba kucha zetu ni muhimu sana kwa miili yetu! Kwa sababu kucha zinabeba dalili mbalimbali za magonjwa , ikiwa ni pamoja saratani. Je umeona sehemu ya chini ya kucha yako, ipo kama mwezi nusu, sehemu hiyo inaitwa lunula, kwa kweli ni eneo la muhimu sana na unapaswa kuhakikisha halipati uharibifu wa aina yeyote ile. Hapa tunakwenda kuelezea mambo matano ya muhimu kujua kuhusu lunula: 1.Sehemu hii inonekana nyeupe,ni basal layer ya tano ya epidemis ambayo inaziba mishipa ya damu ambayo ipo chini. 2.Sehemu hii ya kucha inayoitwa lunula ni mzizi wa kucha na endapo ikiharibika au kuumia kwa namna yeyote ile, basi kucha yote itatoka. 3.Wataalamu wengi duniani kote wamegundua kwamba lunula inaeleza vizuri afya ya binadamu kwa ujumla. Kwa mfano, tiba za jadi za kichina wanaamini kwamba upungufu wa lunula inaonyesha dalili ya upungufu wa damu au utapiamlo, wakati pale au rangi ya blue ya lunula inaonyesha dalili ya ugonjwa wa ki...

Hussein Machozi Adai Kuwa Nafasi yake Kwenye Muziki Bado ipo

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Hussein Machozi amesema kuwa muziki wa sasa unaofanyika ni wa kiki lakini atafanya vizuri kwa sababu nafasi yake kwenye muziki bado ipo kwa kuwa hakuna aliyefanya kama yeye mpaka sasa. Akiongea na Bongo5, Hussein Machozi amesema kuwa nafasi yake kwenye muziki bado ipo kwa sababu hakuna aliyefanya kama yeye mpaka sasa. “Game ni rahisi sana, kwa sababu muziki wa sasa hivi ni kiki. Mimi nitafanya muziki lakini kama ukinambia nifanye kiki nitashindwa,” alisema Machozi. “Siyo kama nitarudisha heshima mimi nina heshima mpaka kesho kwa sababu hakuna mtu aliyeweza kufanya kama mimi. Najiamini najua nafasi yangu bado ipo sema nilikuwa kimya kidogo,” aliongeza.

Sabby Afunguka: AliKiba Alitaka Kuniua kwa Mahaba

Image
MSANII anayefanya muziki na filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kwa kinywa chake kuwa penzi la mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Ali Salehe Kiba ‘Alikiba’ lilitaka kutoa uhai wake kwani hakuna mwanaume aliyemshika mtima wake zaidi yake. Akizungumza na gazeti hili juzikati, Sabby anayedai ana historia ya kutendwa na wanaume alisema kuwa amewahi ‘kudate’ na wanaume wapatao saba lakini kati yao hakuna aliyemdatisha zaidi ya Kiba ila jamaa huyo alitaka kusababisha ajitoe uhai. “Jamani haya mapenzi yaacheni hivihivi, huwezi kuamini Alikiba alitaka kuniua kwa penzi lake, nilimpenda sana na alinidatisha kiasi kwamba nilipokuwa nikihisi ananisaliti, niliumia roho na wakati mwingine kupata presha. “Achilia mbali hilo, kuna wakati nilitaka kujiua kwa sababu yake maana kuna kitu kilitokea, nikaumia sana hadi nikahisi sina umuhimu wa kuishi,” alisema mdada huyo. Inadaiwa Sabby na Kiba waliwahi kuwa wapenzi kwa siri na haikuchukua muda mrefu wakamwagana kwa saba...

Chozi la Mobeto Laana Kwa Lulu Michael

Image
Kufuatia staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kudaiwa kumpora mwanaume aliyezaa naye, chozi la mwanamitindo anayeuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Hamisa Hassan Mobeto linaelezwa kuwa ni laana tosha kwa mwigizaji huyo. Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Mobeto, mrembo huyo ambaye ni sura ya mauzo kwenye matangazo ya nguo za kike, amekuwa akimwaga chozi kila kukicha huku lawama zote akizielekeza kwa Lulu. Chanzo hicho kilidai kuwa, Mobeto amekuwa akilalamika kwamba, Lulu alijua fika mwanaume huyo ni mzazi mwenzake lakini akamchukulia na kumsababishia maumivu ya kutelekezewa mtoto wa kike aliyezaa na jamaa huyo mwaka jana. “Kiukweli chozi la Hamisa (Mobeto) kila kukicha ni laana tosha kwa Lulu. Unajua hakuna kitu kibaya kwa mwanamke kama kuporwa mwanaume wake waziwazi na kuachiwa majukumu ya mtoto huku adui ukimjua. “Kibaya zaidi ni tambo za Lulu mitandaoni. Kitendo cha Lulu kutamba na mwanaume huyo kinamuumiza sana Mobeto kwa sababu nay...

Haya Hapa Maneno Makali ya Diamond Platnumz Kuhusu Ujio wa Wimbo Wake Mpya Baada ya Kukosa Tuzo ya BET

Image
Kwenye mashindano lazima patakuwa na mshindi wa pili na watatu na kukubali kuanguka ni kawaida, ila kuamka  baada ya kuanduka ndio kazi yenyewe ambayo kwa sasa Diamond anafanya kwa  kutoa kazi ambayo yeye anaimani ni bora zaidi baada ya kupoteza tuzo ya BET kwa msanii Black Coffee wa Afrika Kusini. Haya maneno ya Diamond kuhusu wimbo wake mpya aliyoandika Twitter: "Haya Ongeeni Vizuri na waganga wenu Baada ya siku nne simba Anaachia ile Mashine"

Kilichomwangusha Chibu Dangote BET 2016 ni hiki

Image
Ni masikitiko yangu makubwa kuikosa Tuzo hii ya kimataifa kupitia msanii wetu pekee na Brand ya Afrika mashariki. Bila kupoteza muda Na hizi ni sababu zilimfanya Chibu Dangote 1) Hakuwa na kazi inayoeleweka ambayo ingemfanya aongeleke au jina lake lizunguke vichwani mwa watu 2) Kumanage wasanii kwake limekua pigo kubwa maana imemfanya aache kusonga mbele akiamini amefika na ni muda wa kusaidia wengine. 3) Kukosa baraka za mzazi mwenzake mama Tiffah kutokana na usaliti aliomfanyia mwenzake. 4) Kurise up kwa Alikiba. 5) Kuridhika na mafanikio Hivyo Chibu ajipange upya upya ili arudi kwenye mstari.

Mwanamuziki TID na Dully Sykes Katika Bifu...TID Amchana Live Dully

Image
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East AFrica Radio, TID amesema Dully Sykes hakupenda kitendo cha Joh Makini kuwepo kwenye collabo yao ya wimbo wa confidence. “Kwanza ile ngoma mwenyewe ndio alitaka kuwepo baada ya kuisikia, akasema mnyama hii ngoma kali naomba niweke sauti na mimi, nikamkubalia tukarekodi, lakini alivyokuja kusikia Joh Makini yupo akanipigia simu tena usiku, akaanza kunifokea, tena imagine ngoma yangu ananifokea..TID vp unaweka watoto wa Arusha? ndo unafanya nini?” , alisema TID, TID aliendelea kwa kusema kuwa licha ya hilo baada ya kuandaa show ya ku-launch audio, alivyoona na Joh Makini anaperfom, akampigia Joh akimwambia asikubali kufanya show bila kumlipa. “Baada ya hapo akampigia Joh akamwambia Joh ile show kubwa usikubali kuperfom bila kukupa milioni tatu, baadaye Joh akaniambia kwamba bila mkwanja haparfom, nikamuuliza we habari hizo umezitoa wapi? akaniambia ni Dully kanambia, nikamwambia ungejua huyo Dully alimind kusikia we upo kwenye ngo...

Sababu za Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa Kwa Mwanamke

Image
Ni kawaida kwa wanawake kuhisi   maumivu wakati wa kujamiiana. Katika matukio mengi   hali kama hizo, hutokana na mwanamke kutolainika sawasawa, hali hii inaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kuongeza muda wa kumchezea mwanamke(foreplay) au kutumia vilainishi vya ziada. Hata hivyo, iwapo  maumivu hayakuweza kupungua, hizi hapa  ni baadhi ya sababu, ambazo  husababisha  maumivu  wakati wa tendo la ndoa: Kukakamaa kwa misuli ya uke (Vaginismus):  hali hii inasababishwa  na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha. Matatizo ya shingo ya kizazi:  Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi. Iwapo mwanamke ana maambukizi huisi maumivu mara shingo ya kizazi inapogusana na uume. Matatizo katika mfuko wa uzazi:  Matatizo kama fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa ngono. Maambukizi ya uke:  aina yoyote ya maambukizi ya uke kama vile  ma...

Picha:Uwoya Amtia Majaribuni Richie

Image
Irene Uwoya na Richie. WAKATI Waislam wakiwa kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya juzikati alimtia majaribuni msanii mwenzake Single Mtambalike ‘Richie’ walipokuwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar kulikokuwa na harusi ya mdogo wake Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, Happy Mengere. Kwenye ‘mnuso’ huo, Uwoya aliyekuwa amevalia kivazi kilichoacha mapaja yake wazi, alionekana mara kadhaa akimkumbatia Richie na hata paparazi wetu alipotaka kuwafutoa picha, staa huyo alimshika kimahaba na kuwaacha watu wakinong’ona chinichini. “Uwoya hivi haoni anamtia mwenzake majaribuni? Na Mwezi Mtukufu huu analazimisha kupiga naye picha ya kumkumbatia, ila hawa wasanii wamezoeana sana,” alisema mmoja wa waalikwa aliyekuwa karibu na mastaa. Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alipojaribu kuwakaribia na kumuuliza Uwoya kulikoni anamfanyia mwenzake vituko alisema, alijisahau kuwa Richie yupo kwenye Mwezi Mtukufu ila alipiga picha hi...

Mkubwa Fella azungumzia tetesi za Uhusiano wa Aslay na Ruby

Image
Perfecto TV wanatuunganisha na stori zote za Entertaiment ambazo zimechukua Headlines  June 23 2016  na moja kati ya stori za Entertaiment ambazo zimechukua Headlines. Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii hususani instagram, utakuwa ulikutana na post za mastaa wa Bongofleva, Ruby na Aslay ambazO zilileta tafsiri kama wapo kwenye mahusiano, sasa hapa Mkubwa na Wanae Said Fella ametolea ufanunuzi kupitia Perfecto TV.                                                           

Wema Sepetu na ex boyfriend wake ‘Luis Munana’….Wamerudiana?

Image
Wema Sepetu na aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Africa aliyeiwakilisha Namibia Luis Munana , walishawahi kuwa wapenzi suala ambalo halikuwa siri, kwani account zao za mitandao ya kijamii hususani Instagram, zilijieleza lakini baadae waliachana na kila mmoja alifuta picha zote walizowahi kupiga pamoja. Baadae Wema akaweka wazi mapenzi yake kwa mshindi wa Big Brother Africa Idriss Sultan ambaye alikuwa rafiki wa ex boyfriend wake. Baada ya Wema  na  Luis kila mmoja kufuta picha za mwenzake instagram, hawakuwahi kupostiana tena, hadi Alhamisi ya June 23 2016 kila mmoja alipoamua kumpost mwenzake na maneno ambayo hayakueleweka walikuwa wanamaanisha nini.

ZIJUE SIFA ZA MKE NA MUME WA PEPONI

Image
Kabla ya kuliendea somo la leo, hebu tuungalie ulimwengu wa wanaume na wanawake na kuona ni wangapi wanaoacha mabaya ya dunia ili wapate mema ya Akhera. Wanawake wazuri wa dunia  ya leo ambao wangeweza kuwa wazuri zaidi Akhera wameamua kuishi maisha ambayo sio tu hayatawawezesha kuwa na maumbile bora zaidi Peponi bali wana hatari kubwa ya kuikosa hata harufu ya Pepo. Warembo wa dunia wameamua kuutumia vibaya urembo wao na kumpa ushindi mkubwa Ibilisi. Kama kuna fitna kubwa ulimwenguni hivi leo basi fitna hiyo ni “mwanamke”, Zinaa inayofanyika hadharani na faraghani imekithiri Wanawake wamekuwa mtihani mkubwa kwa wanaume. Thamani ya umbile lao wameitupilia mbali, sasa wanaunadi utupu wao mchana kweupe, Ni kazi ndogo na nyepesi kabisa kwa mwanamke wa leo kujiondoshea nguo mwili mzima hadharani, tena kwa fahari. Kiumbe ambaye Mwenyezi Mungu amemuwekea stara nzito ya mavazi katika uhai na umauti wake ndio amekuwa kinara wa kwenda utup...

Kama ni mtumiaji wa YouTube katika simu, wametangaza maboresho mapya

Image
Kama wewe ni mmoja kati ya watumiaji wa mitandao kwa kutumia smartphone yako, basi mtandao wa YouTube umetangaza maboresho katika application yao kwa watumiaji wa simu za mkononi. YouTube wametangaza kuboresha application yao ya YouTube inayotumika katika smartphone, sasa unaweza kuweka video za YouTube live streaming kupitia simu ya mkononi, unachotakiwa kufanya ni kubonyeza button katika simu yako na video unayorekodi moja kwa moja itaenda YouTube.                                                        Maboresho hayo ya YouTube kwa application za simu za mkononi, unaweza ukaifananisha na ile application ya mtandao wa  Periscope na itakuwa na option ya viewers kuweka comment zao kama kawaida. Mfumo huo wa live streaming kwa simu za mkononi wa YouTube unaitwa ‘ YouTube Connect’ ...

VIDEO: ‘Milion 10 usajili wa namba binafsi sio sawa’ Mbunge Kiteto

Image
Baada ya Serikali kupandisha tozo ya usajili wa namba binafsi za magari kutoka milioni 5 hadi 10 kwa miaka mitatu katika bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 , mbunge wa viti maalum CCM Kiteto Koshuma alisimama bungeni kukosoa hatua hiyo kuwa ni kupunguzia mapato serikali kwakuwa itapunguza watu wa kujisajili. ‘ Naamini lengo la serikali lilikuwa ni zuri, lakini ukiangalia wakati kodi ikiwa ni milion 5 watu walioweza kusajili namba zao walikuwa ni wachache, sasa ukisema iongezwe hadi kufikia milion 10 inawezekana tukawapoteza hata hawa ambao walikuwa wakichangia mapato ‘ – Kiteto Koshuma                                                                      

Petit Man: Sipo tena Endless Fame..lakini Sina Tatizo na Wema Sepetu.

Image
Aliyekuwa meneja wa wasanii walikuwa kwenye kampuni ya Endless Fame chini ya Wema Sepetu,PetitMan amesema kuwa kwa sasa hayupo tena kwenye kampuni hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia lakini hata tatizo na Wema Sepetu na kuwa wanaongea kama kawaida. ‘’Endless Fame nilikuwa kama ‘Coordinator’ na pia nilikuwa meneja wa wasanii, kwa sasa hivi nimesimama kufanya kazi Endless kutokana na matatizo yetu ya kifamilia na unajua ile kampuni ni kama familia yangu nimekaa nayo kwa miaka tisa, nimeishi na Wema Sepetu zaidi ya miaka tisa kwahiyo siwezi kusema kitu chochote kwenye media kwa sababu sina tatizo na Wema wala Martin Kadinda, matatizo yametokea upande mwingine, kuna tofauti ilitokea kati yangu mimi na Mirror lakini sasa hivi tuko poa’’ Alisema PetitMan akiwa kwenye kipindi cha Leo Tena.