Simu Mpya Kutoka Tecno, Camon C9 yatua Dar, Ina Kamera ya Hali ya Juu na Mfumo wa Kufungua Simu Kwa Macho

Teknolojia ya simu inaendelea kukua siku baada ya siku, baada ya simu feki kuzimwa na Mamlaka ya Mawasilinao nchini (TCRA), Tecno Mobile imetangaza kuzindua simu kali ya CAMON C9 yenye uwezo wa hali ya juu katika kupiga picha, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za kisasa. Ikiwa simu yako ni miongoni mwa simu zilizofungiwa na TCRA basi ondoa shaka kwani simu hii mpya kutoka Tecno utaipata kwa gharama nafuu kabisa.


Tecno Camon C9 inaanza kuuzwa rasmi tarehe 25 Juni 2016. Unaweza kufanya manunuzi ya awali (pre-order) uwe miongoni wa Watanzania wa awali kujipatia simu hii. Kufanya manunuzi ya awali tembelea exclusive show room za Tecno jijini Dar zilizopo City Mall, Clock tower na Mobile plaza ghorofa ya pili.

Kufanya manunuzi ya awali unahitaji kufanya malipo ya awali ya Tsh. 30,000 ambapo mteja atapata kadi ya “huduma kwa wateja kutoka” Tecno na kifurushi cha zawadi (gift hamper) za bidhaa kutoka Tecno. Kadi ya huduma kwa wateja itatumika katika kutengenezewa simu katika duka zetu za Tecno baada ya kujipatia simu yenyewe.

Mauzo rasmi yanaanza 25 Juni 2016 ambapo watakao kuwa wamefanya pre-order watatakiwa kukamilisha malipo yao dukani hapo na kisha kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya kijishindia zawadi mbali mbali.

Zawadi za Droo

Zawadi ya Kwanza: Samsung LED TV yenye thamani ya Milioni 1.6
Zawadi ya pili: Jiko ya kutumia umeme (washindi wawili)
Zawadi ya tatu: Birika linalotumia umeme (washindi wawili)
Na zawadi zingine nyingi

Kila mteja atakaye nunua Tecno C9 Jumamosi katika First sale itakayofanyka pale City Mall (Showroom inaonekana kwenye picha) atakuwa mshindi. Baadhi ya sifa za Camon C9 itauzwa katika maduka ya Tecno ikiwa katika rangi 3 tofauti na hizi ni baadhi ya sifa zake.

Kama mpenzi wa picha Camon C9 imekupa Camera unaihitaji kwani inaweza kutambua sura na kupiga selfie kali hata ukiwa gizani.

Pia Camera yake ina urembo wa kweli (make-up) ambayo itafanya picha zako kuwa na mvuto wa asili kitaalamu imeitwa
                                           

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Final Exam Answers