Wabunge Wataka Clouds Tv Iadhibiuwe Kwa Kufanya Mahojiano na Kijana Ambaye ni SHOGA


WABUNGE wameiomba serikali kukichukulia hatua kituo cha televisheni, Clouds Tv nchini kwa kukiuka maadili na taaluma ya habari kwa kurusha kipindi ambacho maudhui yake yalikuwa ni kutangaza mapenzi ya jinsia moja.


Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) aliomba Mwongozo kuhusu kurushwa kwa kipindi ambacho kilikuwa kikimhoji kijana mmoja ambaye anajihusisha na vitendo vya ushoga.


“Napenda kuweka maslahi yangu kuwa mimi mwenyewe ni mwanahabari na taaluma hii naifahamu na ndio maana nikaona ni vyema nisimame angalau kupata muongozo wako,” alisema Mollel na kuongeza kuwa sheria ya nchi hairuhusu ushoga kwa maana hiyo kama mwandishi wa habari alipaswa kuzungumzia ushoga, basi angeelimisha jamii kwa kuonesha kuwa kijana huyo anajutia kufanya vitendo hivyo.


Alisema mwandishi huyo angefanya hivyo ili kutoa taarifa kwa wengine kwamba vitendo hivyo sio vizuri katika jamii badala yake kipindi kilihamasisha vitendo vya ushoga na alionesha ni mtu anayefurahia kitendo kile, na jambo la kusikitisha asubuhi hii (jana), mwendeshaji wa kipindi hicho alialikwa katika kipindi cha asubuhi cha kituo hicho, badala ya kuomba radhi ameishia kujitetea.


Kutokana na maelezo hayo, aliomba Mwongozo wa Spika pamoja na Kanuni na kwa kuwa serikali ipo, itoe kauli kama inaruhusu ushoga au kama hairuhusu ni hatua gani inachukua kwa kituo hicho ili iwe fundisho kwa vingine.


Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Maro (CCM) alisema kijana huyo aliyehojiwa na Kipindi cha Take One cha Clouds Tv amewaaibisha wakazi wa Musoma mkoani Mara, hivyo aliiomba serikali imchukulie hatua kwa sababu anaweza kuwafundisha tabia zisizofaa vijana wengine.


Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akijibu miongozo hiyo, alisema jambo hilo linapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016