Mkubwa Fella Atolea Ufafanuzi Tetesi za Chid Benz Kujiunga na Lebo ya Wasafi...Asema Haya

MKURUGENZI wa kundi la Wanaume Family na Yamoto bendi, Saidi Fella maarufu Mkubwa Fella, amesema yeye na meneja wa msanii, Diamond Platnumz, Babu Tale, wameamua kumsaidia mkali wa rapu, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, arudi katika sanaa yake na si kujiunga na kundi lolote.

Fella alisema msanii huyo kwa sasa wamemwanzishia mazoezi maalumu ya kumwezesha kurudisha mwili wake na pumzi ili aweze kurudisha makali yake katika uimbaji bila kuchoka.

Chid Benzi hawezi kujiunga na Wasafi kwa sasa mimi na Babu Tale tumekubaliana tumsaidie yeye kama yeye na si kujiunga na kundi lolote lakini kama anataka kujiunga na lebo yoyote hilo litakuwa la kwake,” alifafanua Mkubwa Fella.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Final Exam Answers