KUFUATIA staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kufunga
ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Helga wiki iliyopita, swahiba wake
mkubwa, Ambwene Yessaya ‘AY’ amefunguka kuwa naye yuko njiani.
Akizungumza na mtandao huu, AY anayebamba na Ngoma ya Zigo alisema kuwa
ni jambo jema kwa rafiki na ndugu yake wa karibu (MwanaFA) kufunga ndoa
hivyo imempa hamasa.
“Nimefurahi sana kwa swahiba wangu kufunga ndoa. Naamini FA amefungua
ukurasa mpya katika maisha yake ya kuwa na mwenzake. Nami nipo njiani
kumfuata Mungu akipenda,” alisema AY bila kumuweka wazi mwandani wake
anayetarajia kufunga naye ndoa.
Comments
Post a Comment