The Industry Wapiga kambi SA Kushoot video 4 na Campos, ni ya Navy Kenzo na Tatu za Wasanii Wao

Kutoka Kushoto: Rosa Ree, Aika, Selina, Nahreel na Wildad wakiwa Afrika Kusini

Timu nzima ya label ya The Industry imepiga kambi nchini Afrika Kusini ilikoenda kushoot video mpya.
Si video moja, sio mbili na watu sio tatu – ni nne.

Aika amedai kuwa wapo nchini humo siku ya tano sasa na wanashoot video hizo na Justin Campos.


Video hizo ni pamoja na za kundi lake na Nahreel Navy Kenzo na tatu za wasanii wa The Industry, Rosa Ree, Seline na Wildad.

Sio mara ya kwanza kwa Navy Kenzo kushoot video na Justin Campos. Video za mwanzo ni Game na Kamatia zilizohit si tu Tanzania bali Afrika kwa ujumla.

Kwa kwenda kushoot video nne kwa pamoja, gharama za usafiri za kwenda na kurudi watu watano, malazi ni ishara kuwa The Industry imeamua kufanya kazi. Navy Kenzo walipata shavu la ubalozi wa Airtel hivi karibu hivyo huenda gharama hizo si kitu kwa sasa. Pongezi nyingi kwa The Industry.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016