Barakah Da Prince Afungukia Ujauzito wa Najma Kumkwamisha

MSANII mwenye ‘title’ kubwa kwa sasa ndani ya ardhi ya JPM, Barakah Andrew ‘Barakah Da Prince’ amekanusha juu ya tetesi zinazoendelea kuwa mpenzi wake Najma ni mjamzito na kwamba ujauzito huo ndiyo unaomfanya yeye kushindwa kuachia kazi nyingine.

Akizidi kufungukia tetesi hizo Barakah aliongeza kusema kuwa alipanga kuachia kazi mwanzoni mwa Julai lakini ameshindwa baada ya kupata menejimenti mpya na kwamba kwa sasa kuna baadhi ya mambo wanayaweka sawa hivyo anatarajia kuachia kazi mpya Agosti.

 “Kuhusu Najma kuwa mjamzito kwa kweli hizo taarifa sifahamu na kama upo utaonekana tu maana hicho kitu huwa hakijifichi, hata hivyo wapenzi wa kazi zangu naomba waamini kuwa nipo katika mipango mizuri ya kazi kwa sasa na Agosti siyo mbali, nitatoa kazi nzuri itakayokidhi vigezo vya kimataifa,” alisema Barakah.

Aliongeza kuwa, kwa sasa hayuko tayari kuifungukia menejimenti hiyo mpya inayosimamia wasanii wawili wakubwa kutoka nchini na wengine wa kimataifa.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016