Lulu Michael Kushtakiwa Kwa Makosa ya Mtandao....

Dar es Salaam: Mwigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ yupo mbioni kupambana na mkono wa sheria kufuatia kumvurumishia matusi mwandishi wa habari wa Global Publishers baada ya kumuuliza swali lililotaka ufafanuzi wake ikiwa ni siku chache tangu alipofanya hivyo kwa mwandishi mwingine wa kampuni hiyo.

Ishu hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita ambapo paparazi alimtwangia simu ya mkononi Lulu na kumuuliza kuhusu kuwepo kwa madai kwamba, yeye ni mjamzito na amekuwa akishinda ndani kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, msanii huyo kwa vile sasa ni mama kijacho, amekuwa nadra kuonekana sehemu za hadhara kwa kuwa hataki watu wajue kwa kuwahofia wabaya wake.
“Ndo’ maana sasa kumuona Lulu waziwazi ni ngumu sana, naona yeye na aliyempa mimba (hakumtaja) wamepanga hivyo. Si unajua wambeya wengi, nadhani anahofia macho ya watu wenye vijiba vya roho na wale washirikina, wakimuona isije mimba ikachoropoka kabla ya wakati,” kilisema chanzo hicho.

Sasa kufuatia madai hayo, ilibidi paparazi amtafute Lulu mwenyewe ili kumsikia. Ni suala la kuweka mizani ya habari sawa kwa mujibu wa maadili ya taaluma, kwamba, mtu anapodaiwa kwa habari, lazima apewe nafasi ya kufafanua au kujitetea. Ni haki ya msingi kabisa.
Lakini cha ajabu, Lulu alipopatikana hewani na kusomewa madai hayo, hata kabla paparazi hajafika mwisho, alikuja juu huku akimwaga matusi kwa paparazi:

“Wewe … (jina la mwandishi), sitaki uniulize maswali ya ….. (tusi). Naomba usitake tukoseane heshima tukaonana wabaya jua nakuheshimu sitaki nikutukane halafu tufikikishane mahakamani laivu. Hayo mambo nenda kawaulize haohao waliyokwambia…(tusi).
Paparazi: Mimi nimeagizwa na mabosi wangu nikuulize…
Lulu: (akadakia) wewe na hao mabosi zako….(tusi).

KUTOKA KWA MHARIRI
Kufuatia matusi yake hayo ambayo hayaandikiki gazetini, paparazi wetu alikwenda Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kulalamika ambapo mtumishi mmoja alimtaka kurudi Jumatatu (leo) kwa ajili ya kuandika maelezo kwenye kitabu cha malalamiko tayari kwa hatua zaidi.
Kwa Lulu ambaye kujulikana kwake na kuwa staa kulitokana na habari zake kuandikwa kwenye magazeti pendwa, hasa ya Global, amekuwa na tabia ya kuwatukana mara kwa mara mapaparazi wetu huku akitishia kuwapeleka mahakamani. Hufanya hivi kila anapotakiwa kutolea majibu au ufafanuzi habari inayomhusu.

KOSA LA KIMTANDAO
Katika makosa ya mtandao yaliyoanza kufanya kazi nchini Septemba Mosi, 2015, kuna kifungu kinasema; Epuka kumtusi, kumkebehi mtu kutokana na utaifa wake, rangi yake, kabila au dini yake.

TUJIKUMBUSHE
Ishu ya Lulu kuwatusi waandishi wetu si mara ya kwanza kwani mwandishi mwingine wa gazeti hili alilalamika kujibiwa kwa karaha na msanii huyo alipotaka ufafanuzi wa jambo fulani.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 8 Exam Answers