ZIJUE SIFA ZA MKE NA MUME WA PEPONI




Kabla ya kuliendea somo la leo, hebu tuungalie ulimwengu wa wanaume na wanawake na kuona ni wangapi wanaoacha mabaya ya dunia ili wapate mema ya Akhera. Wanawake wazuri wa dunia  ya leo ambao wangeweza kuwa wazuri zaidi Akhera wameamua kuishi maisha ambayo sio tu hayatawawezesha kuwa na maumbile bora zaidi Peponi bali wana hatari kubwa ya kuikosa hata harufu ya Pepo.

Warembo wa dunia wameamua kuutumia vibaya urembo wao na kumpa ushindi mkubwa Ibilisi. Kama kuna fitna kubwa ulimwenguni hivi leo basi fitna hiyo ni “mwanamke”, Zinaa inayofanyika hadharani na faraghani imekithiri Wanawake wamekuwa mtihani mkubwa kwa wanaume. Thamani ya umbile lao wameitupilia mbali, sasa wanaunadi utupu wao mchana kweupe, Ni kazi ndogo na nyepesi kabisa kwa mwanamke wa leo kujiondoshea nguo mwili mzima hadharani, tena kwa fahari. Kiumbe ambaye Mwenyezi Mungu amemuwekea stara nzito ya mavazi katika uhai na umauti wake ndio amekuwa kinara wa kwenda utupu.Muslim-Girl-WallpaperWarembo miongoni mwa Wazungu, Warabu, Waafrika, Wahindi na kadhalika wamekubali ‘kuukosa’ Uhurulayn ambao wangeupata baada ya kufufuliwa laiti wangekuwa watu wema. “Mwanamke hana dini”, huu umekuwa msemo mashuhuri wa jamii ambao unathibitika katika maisha ya kila siku, Wanawake wengi huishi kana kwamba dini haiwahusu kabisa ,Kana kwamba ucha Mungu ni sifa ya wanaume, kana kwamba kuswali ni kazi ya wanaume, na kadhalika. Utafiti mdogo tu wa kijamii unaweza kutoa picha ya jumla ya wanawake kwa mnasaba wa yote hayo.

Kuna ahadi kuwa wanawake wema wa dunia watakuwa pamoja na waume zao katika maisha ya Peponi. Kwamba wataumbwa upya kwa maumbile bora zaidi. Lakini ahadi hii, kwa maisha yanayoonekana duniani, ina dalili nyingi za kutotimia kwa wanawake wengi. Hata waume ambao hutangulia mbele za haki wakiwa katika maisha ya wema na wake zao, nyuma yao husalitiwa, Wajane hubadilika na kupoteza mwelekeo, tena wengine, hata kabla Edda kuisha Sharti la ahadi ya kuendelea kwa ndoa Peponi ni kwamba mume na mke wote wafe haliyakuwa ni watu wema, lakini mmoja akingeuka, ndoa ya Peponi haiwezi kuwepo tena.mustlime-couple24Hivyo, wanawake wanaokengeuka baada ya kufiwa na waume zao wema, hawatakuwa pamoja na waume zao. Hivyo, mume na mke wanaopendana kwelikweli ni wale watakaochagua kuishi maisha ya wema na uchaMungu, vinginevyo, kifo kitakuwa mwisho wa ndoa yao.


Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016