Chozi la Mobeto Laana Kwa Lulu Michael



Kufuatia staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kudaiwa kumpora mwanaume aliyezaa naye, chozi la mwanamitindo anayeuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Hamisa Hassan Mobeto linaelezwa kuwa ni laana tosha kwa mwigizaji huyo.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Mobeto, mrembo huyo ambaye ni sura ya mauzo kwenye matangazo ya nguo za kike, amekuwa akimwaga chozi kila kukicha huku lawama zote akizielekeza kwa Lulu.

Chanzo hicho kilidai kuwa, Mobeto amekuwa akilalamika kwamba, Lulu alijua fika mwanaume huyo ni mzazi mwenzake lakini akamchukulia na kumsababishia maumivu ya kutelekezewa mtoto wa kike aliyezaa na jamaa huyo mwaka jana.

“Kiukweli chozi la Hamisa (Mobeto) kila kukicha ni laana tosha kwa Lulu. Unajua hakuna kitu kibaya kwa mwanamke kama kuporwa mwanaume wake waziwazi na kuachiwa majukumu ya mtoto huku adui ukimjua.
“Kibaya zaidi ni tambo za Lulu mitandaoni. Kitendo cha Lulu kutamba na mwanaume huyo kinamuumiza sana Mobeto kwa sababu naye ni mwanadamu. Ana moyo wa nyama kama Lulu

“Pia ukiacha tambo, Lulu amekuwa akisababisha mtoto wa Mobeto anatukanwa jambo lililomuongezea machungu kwani mtoto ni malaika ambaye hajui chochote lakini amekuwa akiunganishwa kwenye ugomvi huo,” kilieleza chanzo hicho.
Alipotafutwa Mobeto hivi karibuni kuhusiana na sakata hilo, hakuwa tayari kumzungumzia Lulu na mwanaume huyo lakini akaweka wazi kwamba kinachomuumiza ni mwanaye kuhusishwa na ugomvi huo.

“Ishu ya Lulu na …(anamtaja mwanaume) siwezi kuizungumzia, kitu ambacho kinaniumiza ni kumwingiza mwanangu kwenye haya mambo. Mtoto wangu anakuwa anajumlishwa katika mambo ambayo hayamuhusu kabisa na hakupaswa kuhusishwa,” alinukuliwa Mobeto na kuongeza:
“Hakuna mzazi ambaye angekubali mwanaye aongelewe kwenye mambo yasiyo mazuri. Ningekuwa sina mtoto wala nisingeumia lakini kwa sababu kuna mtoto ambaye hana hatia wala hajui kinachoendelea hivyo sipendi na naumia sana.”
Jitihada za kumpata Lulu ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS na chatting za WhatsApp hakujibu.

Ishu hiyo ya laana kwa Lulu ilipigiliwa msumari na mama wa marehemu Steven Kanumba alipozungumza na wanahabari wetu hivi karibuni katika futari iliyoandaliwa na mwigizaji Illuminata Poshi ‘Dotnata’, nyumbani kwake, Ubungo jijini Dar.
Alisema Lulu analiliwa na wanawake wengi kwani wapo ambao alikuwa na uhusiano na waume zao wakafariki dunia huku wengine wakiachwa na watoto wadogo na kubaki wakilea wenyewe.

“Lulu ana machozi ya wanawake wengi, Mungu anaona na ninaamini machozi hayo hayataenda bure ipo siku atakuja kuvuna anachopanda kwa sasa,” alisema mama Kanumba pasipo kutaja wahusika moja kwa moja.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Final Exam Answers