Shamsa: Napenda Sana ‘Chupi’ za Mtumba....


Licha ya baadhi ya mastaa kudai wanavaa nguo spesheli tu, tena zile zilizofungwa kwenye nailoni, staa wa filamu Bongo Shamsa Ford amefunguka kuwa, yeye huwa anapendelea kuvaa nguo za mitumba zikiwemo nguo za ndani ‘makufuli’.

shamsaAkizungumzia nguo anazopenda kuvaa, mdada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Terry alisema, kuna mtu huwa anampelekea nguo ‘classic’ za mitumba na anachagua zile zinazomfaa, ananunua na kuzivaa.

“Niseme tu ukweli kwamba, napenda sana nguo za mtumba, hata makufuli. Huwa nanunua, nazifua na kuziweka ‘sopusopu’ kisha navaa, sioni shida katika hilo,” alisema Shamsa.

Serikali iliwahi kupiga marufuku uuzwaji wa nguo za mitumba za ndani kama vile makufuli, brazia na soksi lakini bado nguo hizo zimekuwa ni kimbilio kwa watu wengi wakidai zina ubora na ni za kijanja zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mgando/Mtindi Katika Mwili wa Binadamu