Hizi ni Dalili za Mwanamke Anayekupenda Kwa Dhati Toka Moyoni, ila Hawezi Kukuambia


Kumekuwa na imani potofu kwa wanawake kwamba hawawezi kumwambia ukweli mwanaume anampenda kwanza mpaka mwanaume aanze lakini ukweli usiopingika ni kwamba wao pia hupendi na mara nyingi wao wakianza kupenda hupenda kweli kufikia stage hata ya kuhisi kuumwa. Hizi ni dalili za mwanamke anaekupenda ila anagoma kukwambia tu.

1. KUKUTEGA ILIKUJUA THAMANI YAKE KWAKO
Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda na kumthamini au la mfano wa mambo hayo ni kama kujifanya anaumwa na kauangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake.

2. KUPENDA KUCHEKA TENA MUDA MWINGINE KWA NGUVU
Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli.

3. WIVU
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi na hupenda yale afanyiwe yeye tu hata kama sio mpenzi wako.

4.HUKUMBUKA MATUKIO MUHIMU YOTE KUHUSU WEWE
Anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifauli mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza.

5. HUPENDA KUANGALIANANA WEWE MUDA MWINGI
Eye contact hupendelea sana kukuangalia machon muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utamuelewa ni kiasi gani anakupenda kupitia vile anavyokuangalia. Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda hivyo huweka jicho la wizi na kukuvizia.

6. HUPENDA KUKAANA WEWE MUDA MWINGI NA KUKUJUAZAIDI
Hupenda kukaa muda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe na akikaa na wewe hupendelea sana mwanzoni kukujua wewe zaidi na hukujengea mazingira ya wewe uwemuwazi ili umwambie mengi kuhusu wewe na pia akiwa na wewe atakuwa muwazi zaidi hadi mavazi aliyovaa hupenda sana kujua yako na kukuambia yake na hupenda kujua ni mavazi gani yeye akivaa anakuvutia zaidi na atajitahidi kuwa anavaa ya style hiyo kukufurahisha.

7.YUPO TAYARI KUJISACRIFICE
Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utamuona vipi huyo msichana alivyo kwako na kwa wengine. Yaani yupo tayari akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwambia hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.

8. HUPENDA KUTATUA MIKWARUZANO YENU KWA AMANI
Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakwambia nakupenda.Kwa kuwa anakupenda endapo ikitokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose.

9. HUPENDA KUKUNUNULIA ZAWADI ZA MITEGO
Mwanamke anaekupenda hupenda kujua mengi sana kuhusu wewe na hapo inamsaiia kukununulia zawadi za mitego kama boxer , na mara nyingi hupenda rangi nyeupe, au kukununulia perfume , sabuni ya kuoge ya manukato,soksi, vest, bukta, saa,raba, t-shirt. Na kama mkitoka wote mkaenda shopping ataakutega kwa kukuonyesha vitu na wewe ukionekana umependa kitu hatonunua siku hiyo ila atanunua siku inayofuata na kukuletea kama suprise.

10. KUPENDA MLE WOTE
Mwanamke anaekupenda ili akujue zaidi hupendelea msosi mle sehemu mmoja na kama ikitokea mwanaume hawezi kuhama sehemu anayokula mwanamke yupo radhi kubadili na kumfuata mwanaume hatakama sehemu hiyo yeye haipendi na kama unakula kwako basi atakutega na kuja kupika kwako ili mle na atakuwa anapenda kununua vitu vya kupika ili tu akutekena uone upendo wake.

Ukiona Dalili kama Hizi Mwanaume Tafadhali Fanya mpango wa kumweka ndani (oa) Mwanamke huyo kabla ujachelewa alafu ukaja kuangukia kwa wale wanawake wenye sifa ya Pasua kichwa!!!!

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016