Siwezi Kumuomba Msamaha Chidi Benz Kwa Kauli Yangu ‘Acha Afe’ – Dudu Baya

Msanii mkongwe wa muziki, Dudu Baya, amesema hawezi muomba msamaha Chidi Benz kutokana na kauli yake ‘acha afe’ ambayo aliitoa baada ya rapa huyo kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya na kuomba msaada.
Dudu Baya

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya amesema aliitoa kauli hiyo baada ya kuona rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa na watu ambao walijitokeza kumsaidia.

“Siwezi kumuomba msamaha Chidi Benz kwa kauli yangu ya acha afe,” alisema Dudu Baya “Nachoweza kufanya ni kumpa pole kwa matatizo yaliyompata, na ninamwombea dua Mungu ampe nguvu mpya, akili mpya, mwanga mpya. Bongofleva inamwitaji, jamii imemmis, familia yake inamwitaji na inamtegemea. My best rapper, my friend Chidi Benz hakuna wa kukuokoa, jiokoe,”

Chizi Benz kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kukubali kupelekwa Bagamoyo Sober House kumsaidiwa kuondokana na matatizo yanayomkabili.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016