HASARA YA MAPENZI YA KUCHUNGUZANA

 mwanamke

Katika maisha mawazo ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu, lakini hata hivyo matumizi ya akili lazima yawekewe mipaka na isiwe ni kitu cha kawaida Ubongo kuruhusiwa kwenda mwendo mkali kulingana na uwezo wake.

Hebu chukua jukumu la kuutazama ulimwengu huu tulio nao na uangalie uozo wa wanadamu katika kujiheshimu, kisha ujiulize hivi kuna mwanaume au mwanamke ambaye anaishi bila kumsaliti mpenzi wake?  Baada ya swali hilo wachukue rafiki zako unaokunywa nao pombe na kufanya kazi nao kazi uone kama hamjawahi kuoneshana nyumba ndogo, baadaye fumba macho uiulize akili yako kuna asiyesalitiwa?.

Wakati unasubiri majibu endelea kuweka viashiria kichwani mwako kwa kumfikiria mkeo anayemhudumia bosi chai huko ofisini au Muuguzi anayefanya inashangaza kusikia na kuona kuna baadhi ya wanandoa wanaishi kwa kupelelezana kila siku kama askari wakaguzi wa dawa za kulevya. Mke akichelewa kurudi lazima akaguliwe kwanza kama hakutoka kupasha mwili nje, kadhalika mwanaume  apimwe kwa kunuswa kama hakuchepukia nyumba ndogo.

Hivi tulishawahi kujiuliza kuwa tunautumia ubongo wetu vibaya kutafuta ufumbuzi wa mambo ya kipuuzi!? Tunawafuatilia wake zetu maofisini kwao ili iweje? Hatuaminiani kwa nini wakati tumeoana, je mapenzi yana faida gani ndani ya usaliti na kujua kuwa sio wewe peke yako unayefaidi tunda la mkeo au mumeo.

Inashangaza kusikia na kuona kuna baadhi ya wanandoa wanaishi kwa kupelelezana kila siku kama askari wakaguzi wa dawa za kulevya. Mke akichelewa kurudi lazima akaguliwe kwanza kama hakutoka kupasha mwili nje, kadhalika mwanaume  apimwe kwa kunuswa kama hakuchepukia nyumba ndogo.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016