KWANINI SNURA ALITUNGA WIMBO WA CHURA?


Zimepita siku tatu tangia kuachiwa kwa video ya Chura ya msanii “Snura” wakati audio ya wimbo huo ikiwa gumzo kutokana na watu wanavyojirekodi wakiucheza wimbo huo kwa staili tofauti www.mautunduyabongo.blogspot.com imefanya mahojiano na Meneja wa msanii Snura Hemed Kavu maarufu kama HK ambapo amefunguka kuhusu maana ya wimbo huo na kuhusu video hiyo ambayo inaonekana ipo nje ya maadili.HK SNURA MNJ“Wimbo wa Chura umelenga watu ambao wana mchezo wa kuruka ruka katika mapenzi unakuta leo upo na huyu kesho upo na yule ndio watu ambao tumewagusa kwenye wimbo wa Chura, mwanaume au mwanamke asiyetulia katika mapenzi huyo ni Chura”SNURA VIDEOAkizungumzia kuwepo kwa video inayotajwa kutokuwa na maadili HK amesema video hiyo imetolewa kama bonus track na wimbo imetolewa maalum kwa mitandao ya kijamii na sio maalum kwa kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya habari.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 4 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016