Navy Kenzo ni mfano wa kuigwa kwa wasanii waliokata tamaa kwenye muziki

Navy Kenzo ni kundi linaloundwa na wasanii wawili, Aika na Nahreel.

Hakuna asiyejua kuwa Aika na Nahreel ni wapenzi kwa muda mrefu kabla hawajaingia kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva.

Mwanzo kabla ya kutengeneza kundi la Navy Kenzo walikuwa kwenye kundi la Pah One ambalo walifanikiwa kuachia nyimbo kadhaa kama, ‘Ghetto’ na ‘I Wanna Get Paid’.

Aika na Nahreel walifanikiwa kuachia nyimbo kadhaa wakati wanaanza ndani ya Navy Kenzo ambazo hazikufanikiwa kufanya vizuri na kupenya kwenye ngoma za masikio ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva.

Nawapongeza kwa uvumilivu wa muda mrefu, na sasa wanaanza kuona faida ya muziki wao. ‘Game’ ni nyimbo ambayo hawataisahau kwa maisha yao yote. Ujasiri wao wa kuwekeza hela nyingi kwenye video ya wimbo huo na kufanikiwa kufanya video nzuri chini ya Justin Campos ulivifanya vituo mbalimbali vya TV barani Afrika vicheze wimbo huo.

Mwaka mmoja kabla walionekana ni kama wasanii wa kawaida sana na hawatofika popote, lakini ‘no one knows tomorrow’ leo wamekuwa wakubwa na wameshaanza kupata jina Afrika kutokana na muziki wao wa tofauti na video nzuri zinazobamba kwenye TV.

‘Game’ ilikuwa ni direction nzuri iliyoisafishia njia ‘Kamatia Chini’ nayo ikiwa na video kali ambayo inafanya vizuri kwenye chati mbalimbali za TV kubwa Afrika. Mungu hamtupi mja wake, Aika na Nahreel kwa sasa ni mabalozi wa Airtel ambapo wamefanikiwa kuingiza mkwanja mrefu kutoka kwa kampuni hiyo ukiachana na lile dili alilolipata Nahreel ndani ya Coke Studio mwaka jana.

Wasanii wengi wanatamani kufanya kazi kwenye studio za The Industry Music kwa sasa kutokana na hit nyingi zilizotoka ndani ya studio hiyo.

Kama msanii hutakiwi kukata tamaa ukitaka kufanya vizuri na kama kweli una kipaji ukiwasoma Aika na Nahreel hakika utapata nguvu ya kufanya muziki na kuwa na imani utafika mbali. Japo hawajafika mbali sana na pale inapotakiwa lakini kwa hatua walioipiga Aika na Nahreel hakika wanahitaji pongezi. Ni nguvu zao binafsi wamezitumia hadi kufika hapo walipofika leo.

Hongereni Aika na Nahreel, hakika miaka kadhaa ijayo tunategemea kuwaona mkiwakilisha mbali zaidi muziki wetu wa Bongo Fleva.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016