Skip to main content
HISIA NANE (8) HATARI KATIKA MAPENZI
Naomba nikuulize wewe mwenzangu ambaye
upo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye unahisi ndiye sahihi
kwako, ghafla unaingiwa na hisia ambazo katika mapenzi zinakuwa
zinauweka uhusiano wako rehani, Je unazifahamu hisia ambazo ni hatarishi
kwako karibu katika uwanja wa Mtembezi Mahaba na mie somo wako nipo
tayari kukujuza.
1. NASALITIWA
Kuishi katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti
ni jambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo
yake utajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako ama mke/mume kwa sababu
tu ya kuendekeza hisia mbaya, acha kuhisit afuta ukweli.
2. TUTAACHANA
Kuna wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”,
Wanafanya hivyo eti kwa kutafsiri mwenendo usio ridhisha wa mapenzi yao,
Kusema kweli hili ni jambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa
mapenzi.
Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja
tu, la kutafuta sehemu mbadala ya kwenda baada ya kuachana. Usiwaze
kabisa kuachana hata kama mnagombana na mwenzako kila siku.
3. SIWEZI MAPENZI
Baadhi ya wapenzi huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi,Hata
kama hawaja ambiwa chochote kuhusu kuto watosheleza wenza wao faragha
hivyo hukimbilia kujihukumu wenyewe wakati hujaambiwa kama echeza chini
ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo, kama na lolote linalo kufanya
uwe na hofu muulize mwenzio.
4. NINA KASORO
Naamini mitaani wapo watu ambao huamini wana kasoro fulani ndiyo maana hawafikii viwango vya kupendwa kama wanavyohitaji, “Yaani mimi ningekuwa kama fulani ningefurahi sana lakini ufupi wangu ndiyo tatizo.” Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi wanapendwa ile mbaya, Jisahihishe na epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.
5. NITAMUUA
Miongoni mwa hisia mbaya kabisa kwenye mapenzi ni kufikiria
kumuua mwenzako kwa sababu yoyote, “Nikimfumania na mwanaume
mwingine nitamuua.” Mtu anaye tawaliwa na mawazo ya aina hii anajiweka
katika mtego mbaya kisaikolojia wa kuja kutekeleza kile anacho jiapiza
hata kwa sababu ndogo, Usifikirie hivyo maishani mwako.
6. NIMEKOSEA KUCHAGUA
Usijihukumu makosa kwa sababu umeona mpenzi wako ana tatizo
fulani. Fahamu kuwa kasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka mikakati ya
kumuongoza mwezio kuliko kuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea
kumchagua. “Ningejua kama yuko hivi nisingemchagua.” Usiwaze hivi!
7. HATUWEZI KUZAA
Kuna wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu au minne pamoja bila
kupata mtoto hufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa. “Mmm, mwaka wa
nne umepita bila mtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa.” Kwa nini msizae?
Hizo ni fikra zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwaze hivyo? Jipe
moyo kwani kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wa mwaka
mmoja?
8. UNANIDANGANYA
Ipo aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa wanapendwa sana, hukimbilia kusema na kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm unanidanganya.” Atasema
hivyo licha ya kuona mwanaume anavyojituma kumsotea na kumuonesha kila
dalili za mapenzi. Hili ni jambo baya, ukithibitisha kwamba unapendwa
usihisi unadanganywa, utapoteza bahati yako.
Comments
Post a Comment