Nay Aliachwa na Shamsa Ford Sababu ya Vibomu-Niva


Msanii wa filamu nchini Niva Super Mariyoo, ambaye alionja joto ya jiwe kwa muda fulani baada ya kutajwa kwenye wimbo wa Nay wa Mitego 'Shika adabu yako' na kusema "Huyo msanii huyo hana hata chumba cha kupanga ila anaishi kwenye gari".

Niva amefunguka na kusema kuwa Nay wa Mitego siku zote huwa anaimba watu maarufu ili apate kiki na kusema msanii huyo kutokana na kufanya nyimbo mbovu mbovu ndiyo maana hata siku moja hajawahi kupata tuzo.

Akizungumza kwenye kipindi cha eNEWS Niva Super Marioo amedai kuwa ni kweli kwa sasa wanawake wengi wanafanya kazi na kutafuta riziki na wanakuwa wanawasaidia baadhi ya wanaume ambao kazi yao kukaa nyumbani kama Imma Chogo ambaye ni (Nay wa Mitego).

"Kimaisha mimi Imma Chogo hajanifikia sema sisi wengine huwa hatupendi kujiweka wazi sana, kama kweli mtu unamiliki nyumba, una kwako kwanini hutulii na familia? kama kweli wewe unajiona ni Gentle Man kwanini wanawake wanakukimbia? Star anakimbiwa? mimi najua Star anakimbiliwa. Mimi silelewi bali napewa mahaba ya dhati na mwandani wangu". Alisema Niva
"Mimi namkubali sana Shamsa Ford sababu aliona kabisa yeye ni classic sana kuliko Nay wa Mitego na ndiyo maana hajadumu naye akaachana naye, Nay wa Mitego tatizo haudumii na ndiyo kesi kubwa na Shamsa. Shamsa alikuwa akitoka kupiga movie lile bwana mkubwa linaanza kulialia oohh mara gari halina mafuta mara sijui nini, sasa yeye muziki wake yeye kweli kabisa kwanini anashindwa kumnunulia hata vitu anajinunulia mwenyewe" Niva aliongezea.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016