Mtoto wa Miaka Miwili Amuua Mama yake Kwa Risasi

Mtoto mwenye umri wa miaka miwili amemuua mama yake mzazi kwa bahati mbaya katika jiji la Milwaukee nchini Marekani, baada ya kuikuta bastola nyuma ya gari walilokuwamo.

Mwanamke huyo kwa jina la Patrice Price alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye anafanya kazi za kiusalama nchini humo.

Polisi wa Milwaukee wamesema kuwa mwanamke huyo alipigwa risasi moja mgongoni ndani ya gari hilo ambalo pia kulikuwa na mama wa Prince ambaye ni bibi wa mtoto huyo pamoja na mtoto mwingine wa mama mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mwezi mmoja uliopita mtoto mwenye umri wa miaka minne huko Florida alimpiga risasi mama yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Jamie Gilt katika tukio linalofanana na hilo japo mama huyo hakupoteza maisha.

Pichani ni marehemu Patrice Price

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016