Ni Kweli Kanye West Alilazimishwa Kupiga Picha na Diamond?

Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu Diamond na Kanye West walipokutana kwenye uwanja wa ndege, Los Angeles nchini Marekani na kupiga picha ya pamoja.


Hivi karibuni maneno yameanza kuzuka tena mitaani kuhusu picha hiyo waliyopiga Diamond na Yeezy. Watu wanazungumza kwanini alinuna kwenye ile picha?

Akiongea kwenye stori tatu ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA Radio, Diamond amesema, “Nafikiria ni attitude ya Kanye ndivyo alivyo.”

“Ananuna hata akipiga picha na mkewe na mkwe wake, nafikiria nilipata bahati kwenye ile picha yangu kidogo alifurahi. Kuhusu collabo chochote kinaweza kutokea tumuombe Mungu. Naposema nataka muziki wetu upenye Marekani ni kujaribu kwenda kupambana na wale manguli wao ili tuone itakuwaje,” aliongeza.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016