SABABU ZA KUPENDA ‘DOGODOGO’

age gap relashion ship12345

Katika ulimwengu wa mapenzi kuna mambo kadha wa kadha yanayo weza kusababisha watu wazima kuamua kuingia kwenye mahusiano na watu wenye umri mdogo.

Katika tasnia ya filamu na muziki Tanzania kumekuwa na ‘couple’ ambazo wamezidiana umri na kupelekea baadhi ya mashabiki na watu wa kada mbalimbali kuuliza maswali mengi kulikoni?

Mastaa kama wenye umri mkubwa  (kwenye rangi nyekundu) kama Shilole na Nedy Music, Khadija Kopa na Marehemu Jaffar Ally, Rihama Ally na Leo Masterio, Diamond na Zari licha ya kuzidiana umri waliamua kuingia katika mahusiano ambapo mengine yamedumu na kuota mbawa.Shishi-na Nedy Music

Leo katika ulimwengu wa mahaba mautunduyabongo.com inakudadavulia sababu za watu wenye umri mkubwa kupenda kuwa kwenye mahusiano na watu wenye umri mdogo na kinyume chake.

 Kwanza kabisa URAHISI WA MAISHA Vijana wengi wakileo wanapenda mteremko; mara nyingi hupenda maisha ya bwerere yaani mteremko pasipo kujishughulisha. Mara nyingi hupenda vya bure na kuamua kuingia kwenye mahusiano na mtu aliyemzidi umri kupita kiasi na hii inatokana na baadhi yao kuwa katika hali ya ugumu wa maisha.

 Kama wasemavyo vijana wa karne hii kwamba pesa ndio kila kitu PESA imekuwa na ushawishi mkubwa katika suala zima la mahusiano. Mabinti wenye umri mdogo wamejiingiza katika mahusiano wa wanaume wenye umri mkubwa sambamba na vijana wakiume wenye umri mdogo kupenda kulelewa na wamama waliowazidi umri ili kujipatia pesa.age gap relationship00

Sababu nyingine ambayo imetajwa na wataalamu wa mahusiano inayopelekea watu waliozidiana umri kuingia kwenye mahusiano ni pamoja na KUEPUKA USUMBUFU. Hapa mabinti wengi huamini njia pekee ya kuepuka msongo wa mawazo katika mahusiano ni ‘kudate’ na wanaume wenye umri mkubwa kuliko wao kwa kuwa wanaamini hawapepesi macho kama vijana wenye umri sawa na wao. Pia wanaamini wanaume wenye umri mkubwa hawana wivu wala muda wa kuwa fuatilia nyendo zao kila mara.

Wasichana wakileo hupendelea mahusiano na watu wazima kwa sababu ya UHITAJI WA MTOTO kwa kuwa na hakika ya kuwalea kutokana na uwezo wa kipesa walionao. Vijana wa kiume wa nyakati hizi huepuka kuzaa na mabinti kwa kuwa hawapendi majukumu, hupenda starehe ndio maana hupendelea kulelewa.

Uchunguzi umebaini wanawake wenye umri mkubwa kupenda mahusiano ya kimapenzi na vijana wadogo wakiume kwa sababu ya KUFUATA RAHA YA PENZI ambayo inadaiwa kuwa wanaikosa kutoka kwa waume zao halikadhalika Inasemekana wamama hupenda vijana ambao damu inachemka ili kufurahia raha ya penzi. Age gap kris-jenner-boy-toy__oPt

Moja ya sababu zinazo pelekea mwanamke ama mwanaume kuamua kuwa na ‘kidumu kidogo’ ni MALUMBANO NDANI YA NDOA yaliyo sugu. Magomvi na kero zinazoibuka siku hadi siku husababisha mwanamke/mwanaume  kutafuta binti ama kijana mbichi atakaye mtuliza moyo na kumsahaulisha machungu anayo yapata ndani ya ndoa.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016