Mr Blue Aibuka na Kumtuhumu Mh Sugu Kumuibia Wimbo wa Freedom..Ushahidi Kamili Huu Hapa
Msanii wa Bongefleva ambaye jina lake lilianza kushine kwenye game ya
muziki wa Bongofleva toka akiwa na umri mdogo Mr. Blue, amerudi kwenye
headlines baada ya kupost kupitia account yake ya instagram na kuelezea
hisia zake kuhusu wimbo mpya alioutoa Mr. II Sugu kuwa ni wimbo ambao
alimshirikisha na anashangaa kuona mambo yapo tofauti.
Katika post ya instagram Mr. Blue aliandika
Katika post ya instagram Mr. Blue aliandika
“Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli ..!! SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia ..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa “Freedom” tulifanya pale kwa makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia..sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn…mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu….????”
Comments
Post a Comment