AJALI: Mtumbwi waua watano Kigamboni baada ya kuzama usiku wa May 27 2016
Jioni
ya May 27 2016 kulitokea ajali ya Mtumbwi uliozama Bahari ya Hindi,
watu waliokuwa kwenye mtumbwi huo walikuwa wakivuka kutoka soko kuu Feri
kuelekea Kigamboni Dar es salaam. Mtumbwi huo unasadikika kubeba watu
zaidi ya 16 ambao baadhi yao wametoka wazima.
Siku
ya jana Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanikiwa kuwapata watu nane
ambapo mmoja wao alipoteza maisha. kutokana na changamoto ya giza
shughuli ya uokoaji iliahirishwa na ikaendelea leo May 28 2016 ambapo
miili mingine ilipatikana na kufikia jumla ya miiili ya watu watano.
ULIIKOSA TAARIFA YA GARI LILILOZAMA DAR ES SALAAM APRIL 20 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Comments
Post a Comment