PICHA 25: Kwa Mabachela na wenye hela zenu mnaopenda nyumba za kifahari na mnaopenda nyumba ndogo
Kikubwa
ambacho kimenivutia hapa kwenye hii picha ni baraza isiyo na nguzo
nyingi lakini pia aina ya sakafu ya mbao iliyotumika, ni sehemu hata
ukiamua kujilaza chini au kukaa unajisikia vizuri.
Nyumba
bila madirisha ya chuma na milango ya chumba inapendeza sana sema ndio
basi tu huwezi kujanga kwenye mazingira yetu labda uwe na ulinzi mkali
na wa uhakika wa uzio, sio kwamba Tanzania hamna nyumba kama hizi…. zipo
sema kwenye yale maeneo wanayokaa watu wenye nazo kwa sana.
Huyu hakutaka mbwembwe baada ya kuiweka TV yake.
simple lakini iko poa sana
Ukishazitazama zote hizi usiache kuniandikia ni nyumba au kipisi kipi kimekuvutia zaidi mtu wa nguvu na nitakujibu kwenye comment
Kwa wale wenzangu ambao bado tumepanga kwenye nyumba ndogo, kochi kama hili linatutosha kabisa na bado sebule inakua poa
Kwenye
hii picha hapa inanifanya niwaze kila wakati kwamba nyumba nzuri sio
lazima uwe na mamilioni, kama ndio kwanza unatafuta maisha ukiwa na
nyumba kama hii yenye kochi moja, jiko dogo kama linavyoonekana hapo na
sebule pembeni mchezo umeisha tena imekaa kijanja sana.
Yani hii nyumba jamaa wametumia akili na nafasi ndogo waliyonayo lakini imependeza sana, ramani yake ndio hii hapa chini.
HIZI HAPA CHINI NI ZILE NYUMBA KUBWAKUBWA ZA WENYENAZO….
Huyu aliyejenga hii nyumba alikuja kuangalia eneo kwanza na ramani ikachorwa kutokana na eneo lenyewe, kapatia sana…
Comments
Post a Comment