Je ni Kweli Supu ya Pweza Inaongeza Nguvu za Kiume? Ukweli Huu Hapa
Kwa ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo hili.
Panapokuwa na changamoto Fulani, wajasiriamali huiona changamoto hiyo kama fursa, na fursa hiyo imeonekana kuwanufaisha vijana wanaokaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki la kimataifa la magogoni baada ya supu ya samaki huyo aina ya pweza kuonekana kupendelewa sana na wanaume wa rika zote nchini.
Lakini siku za hivi karibuni hiki kitumbua kimonekana kuingia mchanga, yaani biashara kuharibika baada ya uvumi kwenye mitandao ya kijamii kudai kwamba wakaanga samaki wanaweka dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya viangra ili kuisisimua miili ya wateja wao,
Ni imani ya wanaume wengi wa pwani na hata kutoka bara ambao huishi ukanda wa pwani siku hizi hupenda supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho ambavyo huamini kuwa vinaongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.
Baadhi ya vijana waliozungumza na wamedai kwamba mara nyingi wanatumia supu ya pweza ili kusisimua mwili huku wengine wakidai wanatumia kama kiburudishotu sio kama dawa ya kuongeza nguvu.
ULAJI wa supu ya pweza, kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na chakula hicho.
Kwa siku za hivi karibuni vijana wengi wameonekana kuchangamkia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume bila kushauriwa na daktari
Comments
Post a Comment