NDOA YAVUNJIKA SAA CHACHE KISA ‘KUCHATI’

Kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia kulikofanya ‘kitchen party’ kupata umaarufu katika maeneo mbalimbali na kuwa desturi kwa kila binti anayetaka kuolewa kufanyiwa sherehe hiyo ili aweze kwenda kuishi vizuri na mumewe mara baada ya kuolewa, kwani ni ukweli usiopingika ndoa yahitaji matunzo na mwanaume anahitaji malezi sawa na mtoto.

Mapinduzi ya sayansi na teknolojia yaliyopelekea urahisishaji wa mawasiliano zao lake ni mitandao ya kijamii inayotumika hivi sasa kama vile Whatsapp, Facebook, Twitter na Instagram na yamepelekea magomvi kwa baadhi ya wanandoa kutokana na baadhi yao kutumia muda mwingi ‘kuchati’ katika mitandao hiyo.

CHATTINGHuko nchini Saudi mwanaume mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, amelazimika kuvunja ndoa yake saa chache baada ya kuingia hotelini kutokana na aliyekuwa mkewe kutumia muda mwingi kuchati kwa simu yake ya mkononi wakiwa hotelini kwa mapumziko ya fungate, ambapo mwanaume huyo alimtaka mkewe kuacha kuchati kwa wakati huo ndipo mwanamke akaamua kuweka ngumu huku akimjibu marafiki anaochati nao ni muhimu kuliko mumewe.

Taarifa zinasema mara baada ya bibi harusi kuingia hotelini hapo alianza mara moja kutumia simu yake kuliko kumpa muda mumewe licha ya bwana harusi kujisogeza kimahaba, mwanamke huyo alionekana kutotoa ushirikiano na alipoulizwa alijibu yupo ‘bize’ kujibu meseji zote za pongezi alizotumiwa na rafiki zake baada ya kufunga ndoa, hali iliyopelekea mwanaume huyo kutinga mahakamani kutaka ndoa hiyo ivunjwe kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016