HESHIMA YA MJINI DA’SLAAM NI KUITWA BABA MWENYE GARI ?



LandRover-Discovery 4

Legendari wa Bongo Fleva Tanzania Prince Dully Sykes aliwahi kusema heshima ya mjini Daslam’ ni kuitwa baba mwenye nyumba na sio baba mwenye gari kutokana na yeye kuamini  kwamba gari ni vitu vya kupita lakini unapokuwa na nyumba huleta heshima fulani kwa jamii tofauti na mtu ambaye amepanga lakini anamiliki gari la kifahari.

Imekuwa ada kwa wasanii wa Bongo kushindana kuvuta ndinga kali wakati wanaishi nyumba za kupanga kwa madai kwamba heshima ya msanii itashuka kama wataonekana kwenye daladala na kuamua kujibanza kwenye nyumba za kupanga ili tu waweze kutuna Bongo town na ndinga hata kama ni za mkopo.

ronaldo_cristianoKwingineko duniani katika ulimwengu wa soka wachezaji wenye mitonyo mirefu kama Cristiano Ronaldo na Ronaldinho Gaucho ndio wanaomiliki ndinga kali za mkwanja mrefu aina ya Bugatti zenye thamani ya USD 1,700,000 na hawajaishia kuwekeza kwenye magari pekee pia wanaishi kwenye nyumba zenye hadhi ya juu.

Hapa Bongo Tz Star wa Bongo Fleva anayetuna mjini na ngoma yake mpya ya ‘Namjua’ Shetta ameamua kwenda extra miles na kuwekeza kwenye gari la kifahari aina ya Discovery 3 ambalo kwa ufupi limempa mtonyo mrefu, msikilize hapo chini Shetta akifunguka zaidi.shetta gari

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016