MBINU 4 ZA KUMTONGOZA MWANAMKE AMBAYE HAMJUANI



Unataka kuzungumza na mwanamke ambaye humfahamu?

Kuongea na mwanamke ambaye humjui siku zote inakuwa ngumu kumuingia kwa kuwa lazima utafute pozi la kumuingia kwani huwezi kufahamu ni nani na anafanya nini kwa wakati ule mahali pale ulipokutana naye.

Kile ambacho kinachohitajika kwanza kabisa ni kumfanya mwanamke kama huyo akutambue yaani upate kufahamika kwake. Hii inakuwa rahisi kwa kutumia mbinu hizi.

1. Mtazame
Unaweza kukumbwa na hali hii ukiwa sehemu yenye watu wengi au mkabahatika kukutana wawili tu hapo ndipo hali inakuwa tete lazima uwe na aina ya uangaliaji kwa kuibia kwa mbali sio ukaze jicho hadi akuogope.

Kile unachohitajika sasa ni umuangalie ili ufanye kumuonyesha kama unajaribu kumuangalia yeye. Jaribu kujifanya unamuangalia kisirisiri, halafu akijaribu kukuangalia tu unajifanya unashughuli nyingine ama unaongea na marafiki zako. Hii itamsisimua kutaka kujua kwa nini unamuangalia hivyo itamfanya na yeye kukuangalia mara kwa mara kama utakuwa ukimwangalia.

2. Mwangalie machoni kila wakati akikuangalia, wewe muangalie halafu papo hapo uangalie kando kikondoo. Endelea kumuangalia kimtindo huo mara kwa mara, na wakati mwingine, mwangalie nusu sekunde, uangalie kando halafu hapo hapo muangalie tena. Ukifanya hivyo utakuwa unamsisimua kihisia lakini kama umejaribu njia hii yote halafu hakuonyesha dalili ya kuingiliana basi itakuwa hajakupenda ama kuridhika na wewe.

3. Jifanye kutoeleweka kama upo na marafiki zako, muangalie mara kwa mara, lakini jifanye kama unasumbuliwa na jambo fulani ambalo linakufanya wewe usielewe kile ambacho marafiki zako wanaongea. Hii itamfanya yule mwanamke kufikiria kuwa ameingia kwa akili yako hivyo ataona ya kuwa yeye ndiye chanzo kikuu kinachokuzuia wewe kumakinika na yale ambayo marafiki zako wanaongea.

4. Mwonyeshe tabasamu bila kupoteza wakati,  hii itakuwa ufunguo wa kwako kufungua mlango wako wa kuongea naye kwani akili yake yote  itakuwa imekuja kwako hivyo lile unalohitajika la kufanya ni kumwonyesha tabasamu. Fanya kutabasamu  kiasi tu ili kuonyesha kuwa wewe umevutiwa nae.

Comments

Popular posts from this blog

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mgando/Mtindi Katika Mwili wa Binadamu