TANZANIA IKIPATA DIAMOND 3, MPOTO 3 NA FID Q 3 BAAAAAAAAS!!!!!!!!!! (+Audio)


Jana mautunduyabondo.blogspot.com ilikusogezea karibu baadhi ya wasanii waliopata shavu nchi za nje akiwemo Fid Q na Saida Karoli baada ya ngoma zao kubamba na kutumika nje ya nchi katika filamu na documentary mbalimbali za kampeni dhidi ya ‘albinism’ na tohara.

Pia Super Star wa Bongo na Afrika Diamond Platnumz alipata kushirikishwa katika ngoma ya Cocoa na Chocolate iliyofanywa na wasanii wakubwa Afrika akiwemo D’Banj, Femi Kuti, Tiken Jah Fakoly, Judith Sephuma na wengine katika kampeni ya kuhimiza viongozi wa Afrika kuwekeza katika kilimo kutokana na umuhimu wa sekta hiyo.

AFRICAN ARTISTSasa basi safari hii dili limemwangukia gwiji mwingine wa muziki hapa nyumbani Mrisho Mpoto baada ya kupata mwaliko maalum Ikulu ya Kenya kutokana na ngoma yake ya Deni la Hisani inayopinga ujangili kwa wanyama kumvutia Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na kuamua kumtumia Mpoto katika kampeni ya mapambano dhidi ya ujangili Afrika Mashariki.

mpotoHii inatoa changamoto kwa wasanii wengine hapa nyumbani kuongeza ubunifu na kuumiza zaidi bongo zao wakati wa utunzi na uimbaji ili kupanua wigo wa fursa na kuitangaza Tanzania Kimataifa; msikilize hapo chini Mpoto akielezea namna mchongo ulivyotua kwake.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016