MRIDHISHE MUMEO KWA KUMFANYIA HAYA



couple-breakfast-in-bed2-378x341

Wataalamu wa Mapenzi  wanasema kwamba wamaume ni viumbe rahisi sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo kiasi gani!

Lakini lazima ufahamu kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto Tafuta namna ya kuleta hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata usukani.

Sasa swali linakuja  Nini unatakiwa kufanya, ili kumridhisha mwanaume wako kitandani? Kujibu swali hilo haya hapa mambo 5 ambayo kama yatazizingatiwa kwa makini, basi mwanamke hutokuwa na shida ya kumridhisha mume wako kitandani na nyanja nyingine muhimu za mahaba.

Vaa vizuri. Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi,Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio
tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya mapenzi,vaa nguo laini yenye mtelezo unaomwagika mwilini kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako.

Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana. 
Mwanaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni “innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke, ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya
kujamiiana), isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani.
Wanaume wanapenda wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali.

Fanya mazoezi na onekana Bomba. Wanaume ni watu wakujali sana muonekano wa mwanamke, Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi
kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila nyingi lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna pingamizi katika hilo.

Kuwa Mchokozi. Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi, lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po!

Jiamini na Jipende. Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza unene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba, Hakuna kinacho kera wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016