Good News kwa muziki wa Afrika Chris Brown kampa dili Wizkid
Najua jina la Chris Brown
sio geni masikioni mwa watu wanaopenda muziki, basi leo May 29 2016
huenda ikawa ni good news kwa muziki wa Afrika, baada ya msanii kutoka
Marekani Chris Brown kumpost msanii Wizkid kutoka Nigeria.
Katika ukurasa wake wa Instagram Chris Brown amempost Wizkid na kuandika maneno machache sana, lakini yanatafsirika kama kumualika mkali huyo wa Nigeria katika tour yake ya One Hell Of Nite Tour kwa mwaka 2016 atakayoifanya bara la Ulaya katika nchi za Uholanzi, Ujerumani na Denmark.
Muda mchache baada ya Chris Brown kupost picha ya Wizkid, staa huyo kutokea Nigeria alipost nae picha kama hiyo na kuthibitisha kuwa kuanzia June 5 hadi June 11 2016 atakuwa katika #OneHellOfANiteTour pamoja na Chris Brown.
KAMA ULIIKOSA SHOW YA UZINDUZI WA VIDEO YA ‘HAPO’ ILIYOFANYWA NA JUX, G NAKO NA QUICK ROCKA
Comments
Post a Comment