Wema aweka wazi kuhusu mimba, alivyojigundua mpaka ilivyoharibika ‘nikaona donge la damu likidondoka’
Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Wema alikiri kwamba ni kweli alikuwa ni mjamzito.
“Nilikuwa na ujamzito kweli,” alisema Wema. “Mwezi wa 12 mwaka jana, nilikuwa najihisi kuongezeka uzito, hivyo nikaenda kwa daktari kwa lengo la kusafisha kizazi. Nilipofika kwa dokta nilimwambia hata hivyo nimemisi period, akaniambia ya Mungu mengi pengine nime-concive, nilimkatalia katakata.”
Wema anaendelea kwamba daktari alimshauri akanunue kipimo cha ujauzito ajipime haja ndogo atakapoamka asubuhi na asile kitu chochote kwa ajili ya zoezi la kusafisha kizazi.
“Nilipokuwa narudi nyumbani nilipitia dukani na kununua kipimo hicho na asubuhi nikafanya hivyo, nilishtuka sana, nilikuwa kama nimewehuka nilipoona mistari miwili katika kipimo, siku zote nilizoea kuona mstari mmoja. Nikawauliza rafiki zangu nikiwa katika hali ya furaha baadaye nikampigia daktari nikamwambia nimepima lakini sielewi ninachokiona maana kuna mistari miwili, aliniambia niende na kipimo hicho na akanihakikishia kwamba nilikuwa na ujauzito, sikutaka kumwamini, nikamtaka anipime, hapo ndipo nilipothibitisha, nilisema sasa watanikoma,” anasema.
Baada ya fuhara ya muda mchache akisubiria kupata mtoto, aliona dalili mbaya katika mwili wake.
“Siku ambayo sipendi kuikumbuka ni ile niliyokwenda msalani kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo kisha nikaona donge la damu likidondoka, nilichanganyikiwa kwa kuwa daktari aliniambia sikutakiwa kuona damu. Nilipompigia mama yangu naye alinilaumu sana badala ya kunipa pole aliniambia, ‘Wema nilikuambia mimba haitangazwi!, unaona sasa kilichotokea, niliyajua madhara ya kufanya hivyo!”
Wema alisema alikwenda kwa daktari akiwa na Idris kuthibitisha ni kweli ujauzito ulikuwa umetoka na ulikuwa na wiki 13.
Wema anasema, daktari alimwambia ndugu yake mwingine aliyeambatana naye kwamba ujauzito huo ulikuwa ni wa watoto wawili, yaani pacha.
Comments
Post a Comment