Kiba Apata Mpenzi Mwingine, Asema: Nikimrudia Jokate Nisutwe

Siku chache baada ya kusaini mkataba wa kimataifa na Kampuni ya Sony, Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amedaiwa kufunguka kuwa, kamwe hawezi kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake na akifanya hivyo asutwe mchana kweupe.
kiba na jokateeKiba na Jokate.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini ambacho kipo karibu na msanii huyo kimeeleza kuwa, staa huyo amegundua alipotea njia kwenye penzi la Jokate hivyo hana sababu ya kurudi nyuma kwani huu ndiyo wakati wake wa kufanya mambo makubwa.
“Jamaa tangu asaini mkataba mpya na Sony, hataki kuutia doa. Amesema anataka kutusua kimataifa zaidi hivyo anaona akirudi kwa Jokate ni kama atakuwa amerudi alikotoka kisanii.
“Unajua amejifunza mambo mengi kipindi yupo na Jokate, hataki tena kurudi kule kwani kusaini kwake mkataba mkubwa anataka kuendane na maisha yake binafsi,” kilisema chanzo chetu.
jokate12Jokate Kidoti ‘Jojo’

CHANZO CHAZIDI KUTIRIRIKA
Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, mbali na kula mkataba mnono, Kiba tayari amempata mpenzi mpya ambaye wanaendana kwa kila kitu hivyo anaona ni wakati mzuri wa kufaidi maisha ya uhusiano sambamba na maisha yake kimuziki.
“Ni mtoto f’lani mwenye maadili. Kama unavyojua Kiba ni mtoto wa Kiislamu, safari hii ameona achukue binti mwenye imani kama yake ili aweze kufika mbali maana japo hana mpango wa ndoa kwa sasa lakini anataka mtu ambaye ataishi naye kwa muda mrefu,” kilisema chanzo hicho.

KUFANYA MAMBO MAKUBWA
Chanzo hicho kilizidi kuweka bayana kuwa, Kiba ameapa kufanya mambo makubwa kwani amepata uongozi mzuri ambao unajua kuongoza wasanii na kuwaunganisha na televisheni za kimataifa.
“Kiba kwa sasa ngoma yake inachezwa kimataifa, juzikati kupitia televisheni ya Sound City Africa ambayo makao makuu yapo Nigeria, walitoa saa 12 kwa ajili ya Kiba, wakaiita Ali KibaDay, hapo zilichezwa nyimbo zake tu, ni nafasi kubwa sana ya kujitangaza, imempa connection nyingi za kimataifa,” kilisema chanzo hicho.

DIAMOND ATASUBIRI SANA
Chanzo hicho kilizidi kummwagia sifa Kiba kuwa kutokana na uwezo, uongozi na mkatapa huo mpya, sasa hivi  Diamond atasubiri sana kwani levo zake zitakuwa za mbali.
“Aaah! Diamond atasubiri sana. Kiba anabebwa na vingi kwa sasa, uongozi mzuri na anajua kuimba kuliko huyo Diamond. Ataisoma namba kama unavyosikia wimbo wa Aje ndani ya muda mfupi tu, tayari umekamata,” kilisema chanzo hicho.

MENEJA AFUNGUKA
Baada ya kushibishwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alimvutia waya mmoja wa mameneja wa msanii huyo ambaye hapendi jina lake lichorwe gazetini kwa kile alichodai si mambo ya muziki aliyoulizwa, lakini akaweka bayana kuwa kweli Kiba hayupo tayari kurudiana na Jokate kwani ana mtu wake mpya.
“Hawezi kumrudia, sijui hata amemchukia nini yule mrembo (Jokate). Jamaa kwa sasa ana kifaa kipya lakini hapendi kukiweka wazi. Si unajua naye alivyo mtu wa sirisiri,” alisema meneja huyo.

KIBA ANASEMAJE?
Risasi Jumamosi lilimtafuta Kiba ili kuweza kumsikia anazungumziaje juu ya mrembo huyo na kama kweli hana mpango wa kurudi nyuma hadi kufikia hatua ya kutamka kuwa asutwe kuliko kurudina na mrembo huyo, Kiba alijibu kwa kifupi:
“Haya ni mambo yangu binafsi. Sipendi sana kuyazungumzia. Kifupi wewe elewa kwa sasa siwezi kurudi nyuma, nipo kwenye hatua nyingine za kimaendeleo na namshukuru Mungu nakubalika.”

YA AWALI
Miaka miwili iliyopita, Kiba na Jokate wamekuwa habari kwenye vyombo vya habari wakidaiwa kuwa wapenzi licha ya kwamba, mara nyingie alikuwa akikanusha huku mwenzake akiwema wazi.
Hata hivyo, maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na mlolongo wa kumwagana na kurudiana.
Kuna wakati ilidaiwa Jokate alinasa mimba ya Kiba lakini baadaye ikasemekana kuchoropoka.
Maneno mengi yalisemwa kuwa,  hakuna tumaini la mbele katika uhusiano wao kwa vile, Jokate ni Mkristo, Kiba Muislam huku familia ya mrembo huyo ikitajwa kutokuwa tayari binti yao kuingia kwenye ndoa na mwanaume wa imani tofauti.
Kumwagana kwa safari hii na Kiba kupata kifaa kingine kunahitimisha ‘kapo’ yao iliyodumu kwa miaka mitatu sasa.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016