Wolper Afungukia Penzi Lake na Harmonize, Adai Hakujua kama ‘Mkongo’ Ana Mke

Mwigizaji Jackline Wolper jana amefanya mahojiano na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha TakeOne na kuzungumzia mambo mengi kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake Putin ‘Mkongo’ aliyemvisha pete, na uhusiano wake na msanii Harmonize.


‘Ni kweli Raj (Harmonize) ni mpenzi wangu,ukweli nilimjua siku nyingi nilikuwa nikimchukulia kama mwanamuziki tu, tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa’’ alisema Jack.

’Nisingependa kumuongelea mwanaume niliyekuwa naye ‘Putin’, nikiona picha zake,nikisikia jina lake yaani kuna vitu nikiviona kuhusu yeye naumia sana , na mimi nikimpenda mwanaume nampenda kutoka moyoni, nilijuana naye mwaka 2012 nilikuwa namzungusha kwasababu watu walikuwa wakiniambia kabila lao ni waongo, sasa kipindi alivyorudi hapa nchini alinikuta nipo singo, nilikuwa sipo sawa’’

‘’Katika maisha yangu sijawahi kumpeleka mwanaume kwa wazazi wangu nilimuamini nikampeleka kwetu na unajua mwanaume yeyote unayempeleka kwenu hutokubali kuachana naye kwasababu utakuwa unawaangusha wazazi wako na familia yako na ikiwa wamempokea vizuri lakini kwanini nimekubali kumuacha’’(analia)

‘’Ni kweli alikuwa mume wa mtu, baadhi ya watu walikuwa wakiniambia na kunitumia picha siku ambayo alinivisha pete, n asiku ambayo alinivisha pete nilikuwa sijui ilikuwa ni sehemu ambayo tulikuwa tunapenda kukaa na kunywa kila siku ananivisha pete nikakubali baada ya kunivalisha watu wakawa wananiambia kwanini nimevishwa pete na mume wa mtu sikutaka kumuamini mtu kwa sababu mahusiano yangu mengi yamekuwa yakiharibika kwa sababu kuwasikiliza watu, niliziona picha za harusi lakini nilihisi ni harusi tu, sikuelewa kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi’’

‘’Putin alikuwa akinidanganya kuhusiana na mke wake na niliamini ndoa nyingi watu wanaoana na kuachana na aliniambia ni kweli alikua na mwanamke lakini waliachana, lakini mwanamke aliyekuwa naye ni tofauti na watu walivyokuwa wakiambia yeye aliniambia kuwa hawajaoana na mwanamke huyo ila walitaka kufunga ndoa, kiukweli ni mtu ambaye anaweza sana kujielezea alinidanganya sana, nilimuamini sana kuliko wale watu zaidi ya kumi waliokuwa wakinieleza ukweli kuhusu yeye sikuwaamini, na wale waliokuwa wananiambia ukweli hawakuwa wabaya lakini sikuwaelewa kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi tayari’’ (analia).

‘’Nilitoka naye hapa tukaenda South Afrika(analia) tulienda kwa ajili ya kusoma nakumbuka ilikuwa mwezi wa 12 mwaka jana akaniambia ameshalipa kila kitu na ameninulia gari ya kuendea shule,nikakaa miezi mitatu sikusoma lakini wazazi wangu walikuwa wanajua nasoma ilikuwa ni lazima nimsitiri mchumba wangu kwa wazazi wangu nikawadanganya kuwa nasoma, mama yangu alikuwa anampenda sana mchumba wangu lakini baba yangu hakukubaliana na naye, alikuwa akisema kuwa kama atanichukua kunipeleka South Afrika basi akamilishe ishu ya kunivisha pete na kunioa kabisa, akanivisha pete mbele ya wazazi wangu wakakubaliana baada ya mwezi wangeleta mahali ’’ alisema  Jack.

‘’Tulivyofika South Afrika nilikuwa namfanyia kila kitu kama mke wa mtu, nilikuwa namdanganya mama nasoma lakini baada ya hapo nikaona mambo hayaendi kwa sababu kuna siku nilienda salun nikasikia kuwa mke wake naye yupo kule Sauz na alikuwa ananiaga sana anasafiri anaweza akakaa siku mbili au tatu nikamuuliza akaniambia sio kweli yupo Kongo’’ alisema Jack.

‘’Siku iliyofuata alikuja nyumbani akiwa amechelewa, nilikuwa chumbani yeye alikuwa sebuleni ana’preview’ picha nikataka kumpora simu nikamwambia nimeona picha ukiwa na mke wako, na mtoto wako, akaniambia alimkuta mwanamke wake kwa kaka yake akataka kupiga picha naye ndo akapiga, halafu alikuwa anavaa pete ya ndoa nikamwambia siitaki hiyo pete akaiuza, lakini kuna siku alirudi akiwa ameivaa ile pete nikakasirika nikamwambia naondoka akanitupia ile pete kitandani akaniambia nikaitupe chooni’’ alisema Jack.

‘’Kuna kipindi nilikuwa nalewa sana kutokana na stress, kuna siku nilikuwa ‘location’ nilikuwa nimelewa hadi nikazima akapigiwa simu akanifuata akanipeleka nyumbani akanivua nguo zote akaanza kunirekodi na kunipiga picha, lakini nilifanikiwa kuzifuta, lakini baada ya wiki mbili alinitumia meseji na kunitisha kuwa kitu atakachonifanya watanzania watafunga macho na sitoamini’’ Alimalizia Jack

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016