IJUE MBOLEA YA PENZI




Maneno mengi hutokea pale wawili wanapopendana, hisia za mapenzi ni kitu ambacho hakizuiliki penzi litakaloshikilia upendo ipasavyo hunoga na kuwafanya wenza kutosikia wala kuambiwa dhidi ya mapenzi yao.

Matendo mbalimbali yanayofanywa na wale wapenzi moja kwa moja huchochea upendo wa moyoni ambao hudumu milele, ndio hapo utasikia keshapewa madawa, mara mke wake kamkalia kila atakachoomba lazima apewe na mengine  mengi ambayo umekumbana nayo au kuyashuhudia kwa watu wengine.

Hebu fanya haya tuone kama uhusiano wako utafeli

• Kusikiliza na kuwa mshauri mwema kwa mwenzako. Iwe ni kuhusu familia yake au mipango yake ya baadaye au kimasomo, kikazi na hata kibiashara. Ikumbukwe kuwa mafanikio ya mmoja ni chachu ya maendeleo mazuri  hata mtakapokua katika familia.

• Kujishusha panapotokea kutokuelewana (yaani kuwa mwepesi wa kuomba msamaha),majibizano siku zote hayajengi hasa mnapokuwa mna hasira au mmoja kati yenu ana hasira.Black-Couple-Arguing-in-Bed

•Sema Asante, Neno ahsante ni dogo sana ila lina thamani kubwa sana, ukipongezwa na hata unapopewa pole shukuru. Unapopewa chochote na mwenzako iwe ni ushauri, maoni, mawazo mapya juu ya miradi mbalimbali au kazi huna budi kushukuru.

•Mwepesi wa kusamehe na kusahau. Vilevile mwelekeze mwenzako pale alipokosea ili siku nyingine kitendo hicho kisitokee. Usiwe mwombaji mzuri wa msamaha huku wewe hautoi.

•Msifie mwenzako anapopiga hatua ya maisha anapokua katika muonekano mzuri n.k Usisubiri jirani amwambie. Tena hapa muwe makini sana maana ni rahisi kwa mwingine kuvutika upande wa pili kwa ajili ya kusifiwa (Kusifia kunajenga  picha ya kujali) japokua sio wote wanamaanisha.

•Usisubiri matukio maalum ndo utoe zawadi, kama vile birthday, Valentine day  n.k, mpe wakati wowote unapokuwa na uwezo wa kumpa.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016