BIASHARA YA KUUZA MIILI YAWEZA KUWA CHANZO CHA MAPATO KWA TAIFA?


biashara ya ngono

Biashara ya kuuza miili imezidi kujizolea umaarufu duniani kote ambapo Machi 16 mwaka huu Mahakama ya Juu nchini Botswana ilikataa jaribio la serikali na kutupilia mbali Kundi la Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja LGBT kwa madai ya kuwa wanavunja katiba ya nchi hiyo.BOTSWANA

Huenda hatua hii ya Mahakama ya Botswana kuitaka serikali iwatambue wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ndio sababu iliyowapelekea wakazi wa Majengo B na Fisi mjini Mpanda mkoani Katavi kuitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.

Moja ya madai yao makubwa ni kwamba wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali. “Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini”. Alisema mmoja wa wafanyabiashara hiyo ya ngono.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi.

Suala la kuuza miili linapingwa vikali na viongozi wa Tanzania kwa madai ya kuwa ni kinyume na maadili na kuwa zipo kazi nyingi za kufanya tofauti na hiyo ambayo imeonekana kumdhalilisha mwanamke.

Hivyo operesheni mbalimbali zinaendelea kuwaondoa wanaofanyabiashara hiyo ikiwemo operesheni ya safisha Wilaya ya Kinondoni chini Mkuu wa Wilaya Ally Salum Hapi ambapo wamefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani machangudoa 52.


Comments

Popular posts from this blog

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mgando/Mtindi Katika Mwili wa Binadamu