KWA MAMBO HAYA, MWANAMKE HACHOMOKI


Black girlfriend enjoying being serenaded to by boyfriend

Sio kwenye muziki tu ndo tusikie kiki hata kwenye mapenzi napo pia kiki muhimu, leo kupitia utafahamishwa nini cha kufanya ili mwanamke wako asichomoke kwako na uendelee kuwa dereva wa mapenzi kwenye maisha yake hasa pale mnapokuwa  faragha.

 MAANDALIZI
Usikurupuke kaka, kuwa mpole kabla hujaanza  kula tamu ya ndoa, maandalizi ni muhimu sana ili kuweza kumtengenezea hisia zake kwani utakaposhindwa kumuandaa vyema utamsababishia maamivu na kupelekea kukosa hamu ya kushiriki tendo hilo.

MAONGEZI YA MAHABA
Nyama ya ulimi ni tamu kuliko kuku, hata kama huna senti atakusikiliza tu kwani mwanamke hupenda maongezi yenye kumsifia na kumuonesha yeye ni mshindi kwenye kila jambo, hapo sasa utamfanya ajibidishe na vya ufunguni ili aendelee kusikia hizo sifa na wewe utakuwa umepata faida mkaka.

MUULIZE KITU GANI ANAPENDA  MUWAPO FARAGHA
Ni vyema kujua nini mwenzi wako anapenda ili kuweza kurahisisha safari yako ya kimapenzi, hapa mwanaume inabidi usitumie nguvu ya meseji ili kumuuliza, mwanaume mjanja ni yule mdadisi ili kumuwezesha akutamani zaidi na njia pekee ni kujiamini uwapo mbele yake.

UWE WA MWISHO KUMALIZA
Mwanamke huchelea kutosheka kimapenzi hasa pale mtapokuwa faraga, wataalamu wanasema kuwa ni dakika nane (8) ikiwa tofauti na wanaume, mtembezi.com kupitia kipengele cha mahaba kinashauri kuwa mwanaume uwe wa mwisho kumaliza ili umridhishe mwenza wako.

CHA KUONGEZEA NI HIVI
Usilalamike kusema mwanamke yule anatamaa mara nini, hapana punguza malalamiko na uongeze ubunifu na utundu kwenye mapenzi ndo mpango mzima.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016