Jackline Wolper kahojiwa na Zamaradi na kuyaongea ya mapenzi yake na Harmonize
Kwenye Interview hii ndefu moja ya maneno aliyoyasema Wolper ni haya >>> ‘Rajabu (Harmonize) sijamjua hivi karibuni nimemjua siku nyingi sana nilikua namchukulia kama Mwanamuziki tu, kuja kugundua kwamba Rajabu alikua ananikubali siku nyingi tukawa marafiki, alikuja kunitamkia kwamba ananipenda nikiwa kwenye wakati mgumu sana na mtu niliyekua nae‘
‘Tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa hivi toka tumeanza kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, sitaki kuigiza kwenye swala la mapenzi…. nilikua na mtu ambaye nilikua naamini atakua mume wangu na pete na kidole nilimpa lakini haikutokea, swala la familia na Rajabu linakuja‘
‘Mimi kuwa na Harmonize sio maigizo ni kitu kiko serious, najua kuna watu wengine wanasema Harmonize huyo Chokoraa sijui ameimba nyimbo mbili, sasa kama nimeweza kuwa na mtu wa aina yangu alafu amenitenda alafu unakuja kuniambia mtu ana nyimbo mbili eti nisimpende, mimi sihitaji pesa… naweza kuwa hata na mwendesha bodaboda nikambadilisha‘ – Wolper
Ukitaka kuipata full Interview ya Wolper na Zamaradi Mketema bonyeza play hapa chini...
Comments
Post a Comment