Nape: Wema Ametupa Heshima Kubwa, Tutamuweka Kwenye Rekodi zetu
Waziri wa habari, michezo na sanaa Nape Nnauye amesema msanii wa filamu
Wema Sepetu amewapa heshima kubwa kwa ku launch application yake ya Wema
Sepetu ambayo itakuwa inatoa taarifa za Wema.
Aliyasema hayo alipokuwa amehudhuria hafla hiyo aliyodai amehairisha
kuhudhuria vikao vya bunge ili asiikose, pia amesema serikali itamsaidia
na kumtangaza.
Msaniii wa Bongo Movie, Wema Sepetu akifafanua jambo kwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye baada ya uzinduzi wa
huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya
Hyatt Regency jijini Dar.
Comments
Post a Comment