NAMNA 9 ZA KUMPENDA MPENZI WAKO KWA VITENDO



Kama ilivyo mambo mengine kuwa na ubunifu ni suala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa kwenye jamii yenye mfumo dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, ebu tuliite “kupenda kwa vitendo”  huenda sio kwamba hataki bali hajui.

Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa hujui basi jifunzeni wote ili kuwa na uhusiano bora wenye furaha  kwa kufuata haya mambo machache ambayo wanawake wengi huwa hupenda kufanyiwa ili wajue kweli wanapendwa kihisia na vitendo.

  • couple-kissingHakuna kitu wanawake wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa busu mara kwa mara.

Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umemkumbatia na kumbusu hata kama kalala (hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).

  • Mwambie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati, mayai, viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.

Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje baada ya kupata kifungua kinywa.

  • black-couple-embracingOnesha unajali kwa kumjulia hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani.

Ufikapo nyumbani mkumbatie na busu la mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.

  • married-couple-exchanging-giftsMnunulie vijizawadi mara kwa mara, Wazaramo hununuliwa khanga au hereni na mikufu ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti, kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kesi; mwanamama anafurahi kwelikweli sasa wewe fanya kile unachomudu sio kila siku wala kila mwezi.

  • Msaidie kusafisha meza au jamvi mara baada ya mlo wa jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani ‘mna-share’ kufanya usafi ili kuokoa muda.gift

Lolote litakalotokea kila la kheri, lakini hakikisha unambusu na kumkumbatia kabla hujaanza kukoroma.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016