Gigy Money: Niko Kwenye Uhusiano wa Kimapenzi na Gardner Kwa Miezi 6 Sasa

Gigy Money na Mtangazaji Gadner G Habashi

MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo wa Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita.

Gigy mefunguka haya baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.

“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.

Gardner alipotafutwa ili aweze kueleza kuhusu ishu hii alisema:

“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,”.

Comments

Popular posts from this blog

Idriss Sultan Una Uhakika Gani Kama Mimba ya Wema Sepetu ni Yako?

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

Hizi Hapa Faida za Kunywa Maziwa Mgando/Mtindi Katika Mwili wa Binadamu