NIKKI WA PILI AKANUSHA TUHUMA DHIDI YA JOH MAKINI



Don’t Bother yake Joh Makini mkali wa Hip Hop hapa Bongo iliyofanya vizuri nje na ndani ya Tanzania, imezua gumzo kwa mashabiki na wapenzi wa muziki huo baada ya kuwepo na ‘verse’ yenye utata inayozungumzia uwezo wa Joh katika kuandika mashairi.

Kipande hicho Joh anaimba Una Wi-Fi? Wi – Fi sina chief mi niko na wife,unaandikiwa na Nikki? Siijui hiyo kalamu, jomba, naandikia Bic unatoa nyimbo nyingi sikumbuki kutoa nyimbo mi natoaga hit”. Ishu hii iliwafanya mashabiki wa Joh Makini kutaka kujua ukweli kama Nikki wa Pili huwa anamwandikia kaka yake mashairi ya muziki.

Sasa baada ya ishu hiyo ‘kutrend’ maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii leo Nikki wa Pili ameamua kuvunja ukimya na kuiambia mtembezi.com kwamba hizo ni propaganda zinazoenezwa na watu wasio na mapenzi mema kwa weusi.

joh makiniAkasema “Joh Makini anajiandikia mwenyewe lakini sisi kama weusi tukiwa studio tunasaidiana mashairi hiyo ipo wazi mie nimeshasaidiwa sana, kila mtu amekwisha saidiwa … hauwezi kuwa mtu unayejua kila kitu”. 

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016