Msichana Azitanulia Dola Milioni 3.3 Alizowekewa na Benki Kimakosa

Msichana mwenye umri wa miaka 21 na raia wa Malaysia, aliyezitanulia dola milioni 4.6 za Australia ambazo ni takriban dola milioni 3.3 za Marekani alizowekewa kimakosa na benki, anadai alidhani aliwekewa kwenye akaunti yake na wazazi wake ambao nao ni matajiri.


“Wazazi wangu hunipa hela nyingi sana,” anasema Christine Lee Jia Xin kwenye utetezi wake kuhusu swali la kwanini alidhani anaweza kuwa na fedha zote hizo,” gazeti Sydney Morning Herald limeripoti Jumapili ya May 22.

Lee anadaiwa kutumia mamilioni kwa kununua mikoba ya gharama kubwa, vidani vya thamani, nguo pamoja na kupanga kwenye nyumba za kifahari kwa miezi 11 kuanzia 2014 na 2015 kwa kutumia fedha alizowekewa kimakosa na benki ya Westpac. Katika tukio moja msichana huyo alitumia  A$300,000 kwa siku.

Benki hiyo ilikuja kugundua kosa lake pindi Lee alivyohamisha $1.15m kwenda kwenye akaunti yake ya PayPal kwa malipo ya mara 14 kwa siku moja April 7 mwaka jana, Herald limeandika.

Msichana huyo anadai sasa amebakiza A$4,000 tu.

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu wa kozi ya chemical engineering alishtakiwa May 5 mwaka huu kwa kupata fedha hizo kimakosa na kukaa kimya. Lee Jiaxin alikamatwa na polisi akijaribu kuondoka na ndege kwenda kwao Malaysia kwa passport ya dharura.

Westpac ilipewa mamlaka na mahakama mwaka jana kukamata mali zake zote, kumtangaza amefilisika na kuchukua hati yake ya kusafiria. Benki hiyo iliweza kuwapata PayPal wakarudisha A$1.15m.

Baada ya Lee kuacha kwenda mahakamani wala kupokea simu, polisi walitoa hati ya kukamatwa March 6, 2016.

Boyfriend wa msichana huyo, Vincent King alimwekea dhamana ya $1,000 kumtoa jela baada ya kukamatwa May 4. Anadai hakujua kilichokuwa kikiendelea kwa mpenzi wake.

Hakimu amedai itakuwa ngumu kumshtaki kwa kosa la jinai kutokana na benki kumpa yenyewe fedha hizo.

Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016