AJE YAMFUNGULIA DUNIA ALIKIBA


Ni wasanii wachache wanaotumia majina yao ya kuzaliwa mfano Banana Zorro, Barnaba, Amini na Linah Sanga; miongoni mwa majina hayo huwezi kukosa kumtaja ALI SELEHE KIBA kwani naye anatumia jina  la kuzaliwa.

MAISHA BINAFSI

Ali Kiba amezaliwa miaka 29 iliyopita, amebahatika kupata watoto watu Sameer, Samira na Amiya,Yeye ni wa kwanza katika familia yenye watoto wanne Abdul Kiba, Zabibu Kiba na Abuu Kiba,kuhusu staili ya muziki Alikiba anafanya vizuri zaidi kwenye Afro Pop, RnB na Dancer-Pop lakini amewahi kuzungumza kuwa anafanya staili yeyote ya muziki kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwenye tasnia ya muziki.ALIKIBA NA FAMILIA YAKE

MAFANIKIO  KIMUZIKI

Ali Kiba alianza muziki miaka ya 2003, akatoa na ngoma yake ya Njiwa ambayo aliitengeneza studio za G-record kwa mtayarishaji  KGT, Kumbuka wakati huo Gullu Ramadhan Naj ndiye aliyekuwa Manager wake, mafanikio yakaanzia hapo hadi Cinderella iliyotoka 2006 na kumpa umaarufu mkubwa ikabeba jina la album yake ya kwanza.Alikiba (2)

Baada ya hapo nyota ya Ali Kiba iliendelea kung’ara akapata shavu la kufanya ngoma na R-Kelly 2008 katika “project” ya one8 nyimbo iliyoitwa “Hand Across the World” akiwemo 2face Idibia na Fally Ipupa. Hapa Bongo Kiba amewahi kufanya kazi na Bob Junior, Dully Sykes, Mr Blue, Mwana FA, Christian Bella wengine wengi.ALIKIBA ONE8STARSINSTUDIO

ALISIMAMA KWA MUDA MUZIKI

Ali Kiba alikuwa nje ya game kwa  muda wa miaka 3 kwa madai kuwa alikuwa akiwahudumia watoto wake na kujipa muda wa kulisoma soko. Nyimbo yake ya mwisho ilikuwa “My Every Thing”. Baada ya hapo Kiba akarudi tena kwa mbwembwe na mikogo kibao alipotoa ngoma ya “MWANA ikafanya vizuri ikampa tuzo 6 za Kill Music Award na baadae akatoa “Chekecha” pamoja na Christian Bella “Nagharamia” kisha akamaliza “Lupela” kabla ya kutoa nyimbo ya kushirikina na Sauti Soul “Unconditionally Bae”.alikiba sauti sol behind

Katika kudhihirisha ulejendari wa Msanii Ali Kiba Mtangazaji mkongwe wa Tv na redio hapa Tanzania Masudi Masudi aliwahi kusema kuwa Ali Kiba ni mwanamuziki sio msanii kutokana na uwezo wake katika game ya muziki, licha ya hayo kuna ngoma za kushirikiana na wasanii wa ndani na nje zinatajwa ikiwemo ya Navy Kenzo ambayo inasubiria video, Ommy Dimpoz, Mr Blue, Sey Shay wa Nigeria.ALIKIBA &MR BLUE

AJE

Hii ngoma inayosumbua kwa sasa hapa nchini na Afrika kwa ujumla baada ya kuvuja akiwa ameshirikiana na MI wa Nigeria ambapo katika mahojiano yake Alikiba amesem orijino ameimba mwenyewe na verse ya MI ameimba kifaransa huku ikiwa Exclusive katika  vituo mbalimbali vya luninga vikubwa ikiwemo MTV BASE, SAUND CITY NA TRACE.ALIKIBA NA JOKATE

Ngoma hiyo anatarajia kuiachia kesho katika mtandao wa youtube ambapo wadadisi wa mambo wanasema nyimbo hiyo ameimbiwa Jokate Mwegelo ambaye inasemekana ni mpenzi wa Ali Kiba kwa sasa.


Comments

Popular posts from this blog

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 2 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 3 Exam Answers 100% 2016

IT Essentials (ITE v6.0) Chapter 1 Exam Answers 100% 2016