WAKATI Mwisho Mwampamba aliposhiriki kwa mara ya kwanza Shindano la Big Brother miaka ile ya mwanzo wa 2000, Wabongo wengi hawakuwahi kufikiri kama ni kitu ambacho kingeweza kuwasaidia vijana wetu, hata pale dau kubwa la mshindi lilipotangazwa. Wengi walitazama zaidi katika maadili, kwa sababu kulikuwa na mambo mengi ambayo kwa utamaduni wetu, hayakustahili kuoneshwa katika televisheni kama yalivyokuwa yakifanyika. Lakini taratibu wakajikuta wanaliona shindano hilo kuwa la kawaida, lenye ‘kuburudisha’ hasa baada ya ushindi wa Richard mwaka ule wa 2007. Leo hii, vijana wawili wa Kitanzania tayari wameweka kibindoni jumla ya dola 400,000 kutoka shindano hilo, kwani Richard alichukua dola laki moja alipotwaa ushindi na Idriss Sultan, aliyeibuka namba moja mwaka jana, kwa pesa ya madafu, ana kama milioni 500 hivi! Sasa Idriss amekuwa kijana maarufu sana katika jamii yetu, akiwa ngazi moja y...
Comments
Post a Comment