HEKAHEKA: Ajifungia ndani na kujichoma kisu, majirani waelezea kilichopelekea ajiue
September 27 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM Geah Habib amekutana
na hii iliyotokea Tandale jijini Dar es salaam ambapo mwanaume mmoja
amejiua kwa kujichoma kisu, majirani waeleza ni baada ya kugundulika
kuwa ameathirika na virusi vya UKIMWI, millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye Hekaheka ya leo.
>>>’Alikuwa
anaumwa TB alikuwa anatumia dawa na mimi nilikuwa nimekaa naye majira
ya saa 12 akaniagiza vocha, narudi nakuta mlango umefungwa, nikampiugia
simu ikwa inaita tu hapokei’:-Mke
>>>‘Tulianza
kuchungulia dirishani naona mlango kwa ndani umefungwa, majirani
wakachungulia wakaona mtu kalala, ikabidi wanisaidie kuvunja mlango
kufungua tukakuta kisu kipo shingoni’;-Mke
‘walivyoenda
akapima akaonekana ana virusi akamwambia mkewe kuwa mimi mgonjwa, na
leo asubuhi alidondoka ndio akajua hii safari kwa sababu hivi virusi
kwanini vimefikia hivi na vimeniamaliza haraka, watu wakamwambia hiyo ni
hali ya kawaida tu kwa hiyo Mungu yupo, watu wanajiuliza kwa nini
achukue maamuzi ya harakka wakati ukishaanza kutumia dawa unakuwa
vizuri, hata pale tulipokuwa tumekaa tulikuwa tunaongea hivyo’-Jirani
Comments
Post a Comment